Kwanini siku ya Mwezi?

orturoo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2017
Posts
2,947
Reaction score
4,876
Kwa nini Siku ya Mwezi? July 20
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa siku ya kimataifa ya mwezi huadhimisha kumbukumbu ya kutua kwa mara ya kwanza kwa wanadamu kwenye mwezi kama sehemu ya operesheni ya Apollo 11.

Maadhimisho ya siku hii pia yanazingatia mafanikio ya mataifa yote katika uchunguzi wa Mwezi na kuongeza ufahamu kwa umma kuhusu uchunguzi na matumizi endelevu ya mwezi.

Historia fupi
Mwanasayansi Galileo Galilei alichora picha mbalimbali za mwezi wetu mara baada ya kuuchunguza kwa karibu kabisa kwa kutumia darubini yake aliyoitengeneza mwenyewe katika miaka ya 1609 kwa lengo la kutazama yaliyopo huko anga za juu

Katika chunguzi zake aliweza kupata taswira mbalimbali za mionekano ya mwezi wetu kwa ukaribu zaidi kwa kadri unavyopitia katika vipindi vyake mbalimbali wakati uapoizunguka dunia yetu baadhi ya taswira alizozipata na kuzichora ni ( New moon , Full moon , First Quarter and Last Quarter )

Mwanasayansi Galileo ndiye aliyetufumbua macho wanadamu na kuanza kufuatilizia ili kutambua mengi yaliyojificha huko anga za mbali juu ambapo aliweza kutambua uwepo wa sayari zaidi ya moja katika mfumo wetu wa Jua huku awali wanadamu wote walikuwa wakifikiri kuwa ulimwenguni kuna dunia ,mwezi , jua na nyota ni mapambo ya anga basi

#elimuyaanga #ourmoon #astronomy #tanzaniascience
Kwa maelfu ya miaka, ustaarabu wa binadamu umekuwa ukitazama juu angani na kutafakari asili na mafumbo ya mwezi ambao ni satelaiti yetu ya kipekee ya asili. Uchunguzi wa msingi uliowezeshwa na uvumbuzi wa darubini za kwanza ulifungua sura mpya katika ufahamu wetu wa mwenzetu wa angani.

Pamoja na kuzaliwa kwa shughuli za anga, mwezi ukawa mahali pa mwisho pa operesheni nyingi, zikijumuisha ndege za wafanyakazi ambazo ziliacha nyayo za kwanza za binadamu mahali pengine katika ulimwengu.

Juhudi za uchunguzi wa mwezi zinapoendelea kuchukua sura na mipango kabambe, maadhimisho haya ya kimataifa yanatumika sio tu kama ukumbusho wa mafanikio ya zamani, lakini kama ushuhuda wa kila mwaka wa juhudi za siku za usoni.
Karibu kwa mafunzo zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…