Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Nimemsikia Simon Msuva mara kadhaa akisema hana mpango wa kucheza mpira timu za hapa nyumbani. Lakini nikiangalia umri wake sasa anaweza kuwa na miaka 26 au 27 hivi. Kwa umri huo uwezekano wa kucheza Ulaya ni kama haupo tena. Lakini vile vile ukiangalia soko la wachezaji ligi maarufu za Afrika sioni sehemu anayoweza kwenda kucheza.
Msuva tayari amecheza Moroco zaidi ya miaka 4, hivyo sioni uwezekano wa yeye kurudi tena huko hasa ukizingatia ameshitakiana na timu yake ya Wydad. Pia kutokana na kutocheza kwa muda mrefu ni ngumu kununuliwa Misri. Pia ni vigumu wachezaji wetu kununuliwa na timu za Afrika Kusini.
Hivyo kimahesabu hatima ya Msuva ni kucheza hapahapa bongo ili kurudisha makali yake huku akisikilizia fursa yoyote itakayojitokeza.
Pia nadhani kocha mkuu wa timu ya taifa lazima atakuwa anampa shinikizo kutafuta timu ili kulinda kiwango chake. Na timu pekee nayoona ananukia kujiunga nayo ni Yanga. No doubt about that.