Kwanini somo la hesabu limewekewa vitu vigumu bila sababu za msingi?

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Mara hesabu za logarithm mara interagration vitu kibao ambavyo ukija kwenye kazi huku kuanzia za design za miradi na ujenzi wa uhandisi hukutani nazo yaani tunaua vipaji vingi sana ambavyo watu wange buni vitu.

Calculator zipo, excel zipo, format zipo, inputs zipo, akili zipo?
 
Hiyo simu yako janja Kama sio watu kusoma logarithms usingeweza kuitumia.
 
Hakuna kitu kigumu hapo zaidi ya kichwa chako kuwa kigumu kuelewa au wewe kusoma hesabu katika mazingira magumu.

Unalalamikia ugumu wa hesabu wakati hesabu si ngumu, mazingira yako ndiyo magumu.
 
Hakuna kitu kigumu hapo zaidi ya kichwa chako kuwa kigumu kuelewa au wewe kusoma hesabu katika mazingira magumu.

Unalalamikia ugumu wa hesabu wakati hesabu si ngumu, mazingira yako ndiyo magumu.
kusoma hesabu katika mazingira magumu.

Watoto kibao vijijini Wana akili ila hawazi shule mazingira magumu wanawaza tu nyumbani...
 
Hakuna kitu kigumu hapo zaidi ya kichwa chako kuwa kigumu kuelewa au wewe kusoma hesabu katika mazingira magumu.

Unalalamikia ugumu wa hesabu wakati hesabu si ngumu, mazingira yako ndiyo magumu.
Ni tatizo la nani au watunga syllabus? Kwa mfano mimi nimesoma najua hesabu zina errors nyingi kwenye ufanyaji na mfumo wetu mitihani ya mwisho kuamua hatma yako ya elimu.

Inakuwa shida kuna watu watakuwa na uwezo mkubwa sana ila wataaanguka.. Na sasa tunasoma yote hayo lengo huwa nini kubuni vitu mbona kwetu Tanzania hakuna mambo hayo kwa kiasi kikubwa.
 
Uko njwiii!

Pumzika mkuu. Na kesho nayo siku! 😁
 
Hisabati siyo rahisi, lazima ufike level flani ya IQ ndipo utaweza imudu vema.

Hakuna Taifa hata moja duniani ambalo wote wanaweza Hisabati, bali wateule kadhaa.

Kikubwa hakikisha unafahamu kujumlisha, kutoa, kuzidisha na kugawanya tarakimu.

Hayo mengine ya Algebra, Differential equations, Triple integral sijui Topology au Fourier series waachie wengine wahangaike nayo.
 
Hizo hesabu ni muhim sana ukibahatika kusoma masters hasa kwenye decision making ya jambo lolote
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…