Kwanini Stephen Wassira hafai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM

Kwanini Stephen Wassira hafai kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM

gstar

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
790
Reaction score
1,373
Kwangu mimi mzee Stephen Wassira namuona kama ni muimba mapambio na mtu wa kusifu zaidi bila kuweka hoja mezani. Kila kitu kwake ni propaganda kuliko uhalisia.

Kuna mambo mbayo hayahitaji propaganda zaidi yanahitaji kusemewa ukweli, kwa mfano kwenye suala la utekwaji wa watu katibu mkuu mheshimiwa Emmanuel Nchimbi aliongea ukweli na kutibu majeraha ya baadhi ya waathirika lakini msimamo wa mzee Wassira ulikuwa hakuna watu wanao potea ama kutekwa.

Kwa mambo mengi ikiwemo umri wake wa miaka 80 sidhani kama ataweza kufiti kwenye siasa za kisasa ambapo ukosoaji ni mkubwa kuliko kukubaliana na hoja za mwenyekiti bila kuzi challenge, zinahitaji mwanasiasa mvumilivu ambaye anaweza kukubali kukosolewa hadharani kukubali makosa ya kiuongozi na kujisahihisha.

Kama mimi ningeombwa kupendekeza angalau ningemchagua mzee Mizengo Pinda ama mama Ana makinda.

Sitegemei kuona mapya kutoka kwake bali siasa za minyukano zilizojaa propaganda na kukosa uhalisia, hawezi kukaa meza moja na katibu mkuu lazima watashindwana.
 
Kwangu mimi mzee Stephen Wassira namuona kama ni muimba mapambio na mtu wa kusifu zaidi bila kuweka hoja mezani. Kila kitu kwake ni propaganda kuliko uhalisia. Kuna mambo mbayo hayahitaji propaganda zaidi yanahitaji kusemewa ukweli, kwa mfano kwenye suala la utekwaji wa watu katibu mkuu mheshimiwa Emmanuel Nchimbi aliongea ukweli na kutibu majeraha ya baadhi ya waathirika lakini msimamo wa mzee Wassira ulikuwa hakuna watu wanao potea ama kutekwa.

Kwa mamo mengi ikiwemo umri wake wa miaka 80 sidhani kama ataweza kufiti kwenye siasa za kisasa ambapo ukosoaji ni mkubwa kuliko kukubaliana na hoja za mwenyekiti bila kuzi challenge, zinahitaji mwanasiasa mvumilivu ambaye anaweza kukubali kukosolewa hadharani kukubali makosa ya kiuongozi na kujisahihisha. Kama mimi ningeombwa kupendekeza angalau ningemchagua mzee Mizengo Pinda ama mama Ana makinda. Sitegemeikuona mapya kutoka kwake bali siasa za minyukano zilizojaa propaganda na kukosa uhalisia, hawezi kukaa meza moja na katibu mkuu lazima watashindwana.
Age, tuna pool ya vijana na wasomi wengi kuliko wakati mwingine. Why watu wale wale miaka yote?
 
Age, tuna pool ya vijana na wasomi wengi kuliko wakati mwingine. Why watu wale wale miaka yote?
Balozi Nchimbi ni kijana, mama Samia pia hajazeek, Makala pia ni umri wake wa kawaida, sasa unataka chama chote wabaki vijana watupu?! Lazima tuchanganye watu wa rika tafauti.
 
Wazee wangewaachia nafasi hizo vijana, wao wabaki kama washauri tu, ili hata wakiondoka kusiwe na pengo.
 
Back
Top Bottom