- Kuna watu wengi wanapona kwa kutumia dawa za hospitalini pamoja na mitishamba kwa gharama ndogo (ya kawaida) lakini dawa hizi hazisisitizwi popote, yaani dunia imeamua kwenda na chanjo badala ya tiba huku wengi wakiangamia wakati tiba ipo. Je, ni kwamba hizi dawa hazifai?
- Msaada wa chanjo uliotolewa nchini ni dozi milioni 1 lakini idadi ya watu ni milioni 57. Je, kama taifa tumewahi kufikiria kuhusu gharama ya kupata dozi inayosalia ili jamii nzima ichanjwe kuwa itakuwa kiasi gani na itapatikanaje na hivyo kujikita katika kile tunachokimudu kati ya kuchanja au kutibu?
- Kuwepo kwa aina nyingi za chanjo ambazo zingine zinakataliwa na baadhi ya nchi kwamba haziaminiki ni dhahiri kwamba hizi chanjo zinatakiwa kuhuishwa ili kupata aina chache za chanjo zitakazokubalika duniani kote, hivyo siyo busara kukimbilia kitu ambacho hakijapatiwa muafaka.
- Kumekuwepo na tabia ya kirusi cha korona kubadilika badilika, hivyo kupata chanjo moja itakayodhibiti aina zote yaweza kuchukua muda na hivyo watu kulazimika kuchanja tena huko mbeleni.
Ushauri: Kwa kuwa chanjo ni hiyari, Serikali ijikite katika kuangalia dawa bora kati ya dawa zinazotumika kutibu korona na isisitize tiba ya korona badala ya kusisitiza na kuhamasisha chanjo zaidi, ili makundi yote yaweze kukidhiwa mahitaji yao (maana waliochanja pia wanaweza kuambukizwa na kutumia dawa hizo sawa na wasiochanjwa).