Kwanini taifa liwe maskini wakati tuna rasilimali za kutosha

Kwanini taifa liwe maskini wakati tuna rasilimali za kutosha

black and white

Senior Member
Joined
Apr 25, 2013
Posts
102
Reaction score
26
Almasi
Tanzania ni mzalishaji mkubwa wa almasi kwa miongo kadhaa kutoka machimbo ya Williamson, Mwadui ambako uchimbaji wa kibiashara ulianza 1925. Miamba 300 ya kimbalaiti ipo Tanzania na asilimia 20 yake ina sifa za kuwa na almasi.

Dhahabu
Dhahabu ni eneo zuri sana la kuwekeza. Wasaa wa sasa upo kwenye machimbo ya zamani katika mfumo wa miamba ya ukanda wa Archaean Greenstone kando kando ya ziwa Victoria, na miamba michanga ya proterozoki. Uchimbaji wa dhahabu umeongezeka kwa kasi miaka ya 90 kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mbinu mpya.

Mashapo makubwa ya dhahabu yamegundulika eneo la Ziwa Victoria na yapo katika hatua mbalimbali za uchimbwaji. Dhahabu pia imegunduliwa kusini magharibi mwa Tanzania.



Metali za Bezi na Kundi la Platinamu
Kijiolojia, miamba ya Archaean na Proterozoki ina uwezekanao wa kuwa na metali za bezi na kundi la platinamu. Ugunduzi wa hivi karibuni kaskazini magharibi mwa Tanzania umeonesha kuwepo kwa hazina kubwa ya madini ya nikeli, kobati na shaba iendanayo na mfumo wa miamba ya Karagwe-Ankole.
Zaidi ya hapo, kundi la metali za kroniumu na platinamu limeonekana. Hazina kubwa ya nikeli iliyo na ngegu pamoja na kobati imebainika. Kuna akiba ya shaba, fedha na urani mkoani Shinyanga.

Metali za chuma
Mawe yenye madini ya chuma yametambulika kwenye miamba ya proterozoki huko Liganga kusini magharibi mwa Tanzania karibu na makaa ya mawe ya Ketewaka-Mchuchuma. Madini ya titani yanapatikana kwenye mchanga wa pwani ya bahari pia.


Bati na madini ya kutengeneza chuma cha pua
Bati na madini ya kutengeneza chuma cha pua na filameni za taa za umeme yanapatikana Karagwe kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Vito
Tanzania imejaliwa aina nyingi za vito ikiwemo Tanzanaiti inayopatikana kwenye mfumo wa miamba ya Usagara na Ubendi. Tanzanaiti inachimbwa Mererani.Vito vingine vinavyochimbwa nchini ni rubi, rodolaiti, johari ya rangi ya samawati, zumaridi, ametisti, krisoprase, peridoti na tormalini.Hivi karibuni ugunduzi ulifanywa Mkoani Ruvuma, Mtwara na Lindi wa krisoberi, spineli, zumaridi, ganeti, zikoni na almasi.
Mauzo nje ya vito yalikaribia US $ 10 millioni mwaka 1996, na vingi vikiwa ghafi. Kuna nafasi kubwa ya kuwekeza katika usanifu na unakishaji wa tasnia ya vito.

Kaboneti
Zaidi ya kaboneti 20 zinazohusiana na volkano zimebainishwa nchini, na ambazo zimekuwa chanzo cha elementi adimu kama nibimu na fasfati.

Makaa ya mawe
Hazina ya makaa ya mawe iliyo na ubora sawa na ile ya Gondwana Afrika ya Kusini, inapatikana Ruhuhu na Songwe-Kiwira Kusini-Magharibi mwa Tanzania. Jumla ya tani za akiba 1.5 billioni zimegunduliwa. Machimbo pekee ya mkaa wa mawe yapo Kiwira, yenye kuzalisha tani 35,000 kwa mwaka, na yote yakitumiwa hapa nchini kwa kuzalisha umeme.

KALAGABAO
 
Roho mbaya ndiyo maana vyote vilivyo tajwa vipo CHINI..... tusafishe roho vitaletwa JUU !!!!!!
wewe chunguza toka tupate UHURU.
 
swali kashindwa rais we ndo unajidai unamajibu sio?.:mvutaji:
 
Sometimes huwa nakaribia kufikiri kuwa Tanzania iliumbwa ile nchi nyingine zinufaike lakini si Watanzania wenyewe.
 
Subiri kidogo swali lako tutaunda tume ya kuchunguza kwa nini baada ya kufanya upembuzi yakinifu
 
Rasilimali zipi? Wakati tembo kinana amewamaliza,wanyama wengine magamba wanahamishia uarabuni,aridhi wanapewa wageni,madini wamepewa wawekezaji toka nje we vipi?
 
roho mbaya za wachache wenye tamaa, ubinafsi na uroho ndo zinasababisha nchi yetu inazid kuwa masikini, wanasiasa wameiharibu nchi yetu, kwani bila siasa hatutaishi? bora hata niutamani ukoloni kama mch, msigwa labda hali isingekuwa hivi maana kama wakoloni wangezichezea rasilimali hizi leo tusingekua nazo, walitunza thats why tumezaliwa tumezikuta, baba wa taifa aliwahi kusema, kile ambacho hatukihitaji kwa wakati tukiache mpka tutakapokua tayari ndipo tukifanyie kazi, mfano madini, gas, mafuta n.k ni kuviacha tu kwani haviozi mpaka tupate wataalam, sasa tanzania hii ya leo kushnei kabisaa..aaaagh:angry::angry:
 
Back
Top Bottom