Kwanini takwimu rasmi kuhusu uchumi kwa mwaka 2018 bado hazijatoka mpaka leo hii?

Kwanini takwimu rasmi kuhusu uchumi kwa mwaka 2018 bado hazijatoka mpaka leo hii?

PseudoDar186

Member
Joined
Mar 18, 2017
Posts
91
Reaction score
224
Habari za jioni wanajamvi.

Moja kwa moja kwenye mada. Nimefanya kazi moja leo kupitia tovuti rasmi za National Bureau of Statistics (NBS - http://www.nbs.go.tz), Office of Chief Government Statistician, Zanzibar (https://www.ocgs.go.tz/), Bank of Tanzania (BoT - https://www.bot.go.tz/) na Ministry of Finance and Planning (MoFP - http://www.mof.go.tz/). Lengo na madhumuni ni kupata takwimu rasmi juu ya mwendendo wa ukuwaji wa uchumi wetu na kuangalia ni sekta gani katika uchumi zimefanya vizuri na zipi zimepata changamoto. Mimi kwa kawaida ni mfwatiliaji mzuri sana wa masuala ya uchumi – pia nimesomea uchumi, usimamzi wa fedha na uwekeza ngazi ya digrii na masters katika vyuo mbalimbali n’gambo (majina kapuni).

Nikianza na NBS. Hii ofisi kwa kweli ilikuwa hodari sana katika kutoa takwimu za uchumi. Kila robo ya mwaka tulikuwa tunapata ripoti iliyokamilika juu ya mwenendo wa uchumi na udadavuzi (analysis) kutoka timu ya NBS kuelezea “key trends” na mambo mengine katika ripoti hiyo. Hizi ripoti unaweza pata ukifika hapa: http://www.nbs.go.tz/index.php/en/gross-domestic-product-gdp. Mwisho wa kutoka “Quartely GDP Highlights” ni Robo ya Pili ya mwaka 2017 (R1-2017). Swali langu la kwanza ni kwa nini NBS wameacha kutoka hizi ripoti muhimu kwa wakati ili zifanyiwe kazi na wadau?

Sikuishia hapo. Kuendelea kuperuzi tovuti ya NBS, nilikuta ripoti ya NBS ambayo inaelezea kwa kina kuhusu zoezi la kubadili mwaka wa kizio (base year) kutoka mwaka 2007 kupeleka mwaka 2015 ili kuboresha mahesabu ya pato la taifa (GDP). Hii ripoti ilifanya mabadiliko kadhaa katika mahesabu na kuonyesha mahesabu mapya baada ya hichi kizo kubadilika. Ripoti nzima iko hapa http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/na/Revised_National_Accounts_BASE_YEAR_2015_Sw.pdf. Ukisoma vizuri ripoti hii, mabadiliko ya mahesabu siyo makubwa sana – uchumi wa mwaka 2015 unaonekana ulikuwa mkubwa kwa TZS 3.5 trillion (au asilima 3.8) ukulinganisha miaka ya kizio miwili (yani 2007 na 2015). Zoezi kama hili lilifanyika katika nchi ya Nigeria mwaka 2014 – ambapo uchumi ulibanika kuwa NGN 37.8 trillion zaidi (au asilimia 89.2) na kupelekea Nigeria kuwa nchi yenye uchumi mkubwa Afrika, ikiipiku Afrika Kusini.

Hii ripoti ya NBS iligusia kidogo kuhusu ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2018. Ukipita kurasa ya 8 na ya 9, utasoma kipande hichi:

“Mwaka 2018, takwimu za Pato la Taifa kwa Robo mwaka zilizorekebishwa kizio cha 2015 zinaonesha kasi ya ukuaji ya asilimia 7.1 ilikuwa katika Robo ya Kwanza (Januari hadi Machi 2018) wakati kasi ya asilimia 6.3 ilikuwa katika Robo ya Pili ya mwaka (Aprili hadi Juni 2018). Katika Robo ya Tatu ya Mwaka (Julai hadi Septemba 2018) kasi ya ukuaji ilikuwa asilimia 6.8. Kwa msingi huo, wastani wa kasi ya ukuaji katika kipindi cha Januari hadi Septemba, 2018 ilikuwa asilimia 6.7. Kasi ya ukuaji katika robo ya Nne mwaka 2018 itapatikana katika Taarifa ya Pato la Taifa kwa Robo Mwaka inayotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Machi, 2019.”

Kwa muhtasari, R1-2018 – 7.1%, R2-2018 – 6.3%, R3-2018 – 6.8%. Wastani R1-R3-2018 ni 6.7%. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya NBS. Pamoja na kwamba taarifa hizi ni rasmi, swali langu la pili ni kwa nini NBS hawajatoa ripoti iliyokamilika kuhusu ukuaji na mwenendo wa uchumi wa R1, R2, R3 na R4 ya mwaka 2018 kama ilivyokuwa miaka ya nyuma? Hizi ripoti (nimeambatanisha moja hapo juu) ni muhimu sana kwa wadau wa uchumi wa nchi hii na kuandika tu kasi ya ukuaji wa uchumi wa kila robo bila ya ripoti kamili inayoonyesha ukuaji ulitokea katika sekta gani na kwa nini haiwezi kuwapa wadau amani juu ya takwimu hizo. Hii inanileta katika swali langu la tatu.

Swali langu la tatu ni – kwa mujibu wa taarifa rasmi, kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka mzima wa 2018 ni asilimia ngapi? Kama kawaida, nikaondoka katika tovuti ya NBS na kuingia tovuti na Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP). Hapa nilivuta muhtasari wa hotuba ya Waziri Philip Mpango akiwasilisha bungeni makadirio ya mapata na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2018/19 mnamo 3 Jun 2019. Pakua hapa (http://www.mof.go.tz/docs/news/MUHTASARI WA HOTUBA BAJETI 2019 WFM.pdf) Ukifikia ukurasa wa 4, utasoma haya maneno:
“Mheshimiwa Spika, uchumi wa nchi yetu umeendelea kuimarika ambapo mwaka 2018, Pato la Taifa kwa kutumia bei ya kizio ya mwaka 2015 lilikua kwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2017.”

Kwa kuwa NBS iko chini ya MoFP, sina budi kukubali maneno ya Waziri kwamba ni kweli uchumi wetu umekua kwa asilimia 7.0 kwa mwaka 2018. Kinachonikwamisha ni kutopata “ripoti kamili” ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2018 ili kuelewa kwa kina ni sekta gani zilizochangia ukuaji huu. Mpaka hapa nilipofikia, swali la tatu jibu rasmi ni asilimia 7.0 (kauli ya Wizara ya Fedha) ikiwa asimilia 0.3 zaidi ya wastani wa ukuaji wa R1 2018 mpaka R3 2018 (asilimia 6.7, kauli ya NBS).

Nikapitia tovuti rasmi ya Benki Kuu ya Tanzani (BoT) na kupakua taarifa ya uchumi ya robo mwaka (Quartely Economic Bulletin) wa kwanza 2019 (Jan – Mar 2019). Unaweza kupakua mwenyewe hapa https://www.bot.go.tz/publications/QuarterlyEconomicBulletins/MARCH_2019_APPROVED_QEB.pdf.
Ripoti hii ilipandishwa katika tovuti ya BoT mnamo tarehe 23 Mei 2019. Ukurasa wa kwanza wa ripoti hii (ni ya kwanza ya nne zinazotoka kila robo mwaka), katika angalizo la kwanza (“footnote”) kuna maneno ya kushangaza sana. Nimeyaleta hapa uyasome mwenyewe kama bado hujafungua ripoti ya BoT:

“Statistics for the quarter ending December 2018 and March 2019 were not available at the time of publishing this report.”

Kwa kifupi, BoT hawana habari yoyote kuhusu ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa robo ya mwisho ya 2018 na robo ya kwanza ya mwaka 2019 (R4 – 2018 na R1 – 2019). Tukilinganisha angalizo hili na taarifa kutoka NBS katika ripoti ya zoezi la kubadili mwaka wa kizio kwamba “Taarifa ya Pato la Taifa kwa Robo Mwaka inayotarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi Machi, 2019”, unahisi kuna ukakasi kidogo kuhusu upatikanaji wa taarifa za mwaka 2018 na pia, robo ya kwanza ya mwaka 2019. Ripoti ya ukuaji wa uchumi kwa R4 – 2018 imechelewa kwa miezi miwili na takriban wiki moja sasa. Ripoti za R1 – 2018, R2 – 2018 na R4 – 2018 bado hazijatoka mpaka leo hii. Ni zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Sikuishia hapo. Nikapanda boti ya tehama kuelekea Zanzibar kwa Office of Chief Government Statistician kwa kupitia tovuti yao rasmi. Zanzibar wamenishangaza sana. Hawana mchezo na data. Nimepakua Zanzibar Statistical Abstract – 2018 ambayo imetoka Mwezi wa Tano mwaka huu. Unaweza pakua hapa: https://www.ocgs.go.tz/php/ReportOCGS/Zanzibar Statistical Abstract 2018.pdf. Ni ripoti kamili ya takwimu zote muhimu za Zanzibar kwa miaka 5 hadi 10 iliyopita. Ukurasa wa 82, jedwali F1.1 unaonyesha dhahiri kabisa kwamba uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia 7.1 kwa mwaka 2018. Majedwali F1.2 mpaka F1.6 yanakupa picha halisi kuhusu kasi ya ukuaji wa uchumi wa Zanzibar kwa sekta na pia . Hii ripoti imenipeleka kuuliza swali langu la nne – kwa nini Zanzibar wameshafunga mahesabu yao ya 2018 na sisi huku bara bado tunasua?
Upande wa Tanzania Bara, Kitabu Cha Hali ya Uchumi mpaka leo kipo katika chapisho la mwaka 2017 (pakua hapa: http://www.mof.go.tz/docs/KITABU CHA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KWA MWAKA 2017.pdf).

Maneno ya Waziri Mpango yanijitosheleza, ila kama kawaida nikaendelea kufanya uchunguzi wa kina zaidi. Nilipakua ripoti ya International Monetary Fund (IMF) inayohusu mwenendo wa kiuchumi wa nchi kusini mwa jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa Regional Economic Outlook). Unaweza pakua hapa: https://www.imf.org/~/media/Files/Publications/REO/AFR/2019/April/English/sreo0419.ashx?la=en. Naomba nitoe angalizo. Hii ripoti siyo ile iliyovuja – ambayo nimeitupilia mbali. IMF waliikana na Serikali yetu waliikana. Iliyovuja haipo kabisa katika tovuti ya IMF kwa sababu haikutoka rasmi. Hii hapo juu niliyoambatanisha ni ripoti nyingine kabisa. Pia, hii ripoti ni mama yake ni ripoti kubwa zaidi ambayo huitwa World Economic Outlook (data zake ziko hapa https://www.imf.org/external/pubs/ft/weo/2019/01/weodata/index.aspx). Haraka kabisa nikaenda ukurasa wa 58, jedwali SA1. Kwa mujibu wa IMF, ukuaji wa uchumi wa Tanzania mwaka 2018 ni asilimia 6.6. Hii haijatofautiana sana na taarifa rasmi za NBS (asimilia 6.7) za R1 2018 mpaka R3 2018. Ila ni ndogo kuliko ile asilimia 7.0 aliyoitaja Waziri Mpango. Sitaongeza mengi kwa kuwa ripoti yao ilitoka kabla ya muongozo rasmi kutoka Wizara ya Fedha. Ila inashangaza kidogo – IMF na BoT wamechelewa kupata taarifa rasmi za ukuaji wa uchumi wakati hawa ni wadau wakubwa sana wa masuala ya uchumi katika nchi hii.

Nilipitia tovuti rasmi ya Africa Development Bank (ADB) ambao ni washirika wakubwa sana kwenye mambo ya maendeleo hapa Tanzania. ADB kila mwaka wanachapicha ripoti iitwao African Economic Outlook (AEO) ambayo hudadavua kwa kina mwenendo wa uchumi wa nchi za Afrika pamoja na matarajio ya miaka miwili ijayo. Kwa mujibu wa hii ripoti, ukuaji wa uchumi wa Tanzania mwaka 2018 ni asilimia 6.7. Ni dhahiri kwamba ADB wamechukua wastani wa ukuaji wa robo ya kwanza mpaka ya tatu ya mwaka 2018 iliripotiwa na NBS. Pitia hizi repoti mwenyewe hapa ujionee. African Economic Outlook (https://www.afdb.org/fileadmin/uploads/afdb/Documents/Publications/2019AEO/AEO_2019-EN.pdf). Kiswahili pakua hapa (https://www.afdb.org/fileadmin/uploads/afdb/Documents/Publications/2019AEO/AEO_2019_Kiswahili.pdf).

Ripoti ya Global Economic Prospects ya Benki ya Dunia (World Bank) pia sikuiacha. Pakua hapa (http://pubdocs.worldbank.org/en/506...Economic-Prospects-June-2019-Analysis-SSA.pdf). Data katika namna ya Excel nimeziweka hapa kwa wale wanaoweza kutumia Excel kufanya udadavuzi (http://pubdocs.worldbank.org/en/872...omic-Prospects-June-2019-GDP-growth-data.xlsx). Hii ripoti imetoka June 2019 (mwezi huu wa kuandika uzi). Ningependa pia kutoa angalizo ya ripoti hiyo, toleo la January 2019 (pakua hapa http://hdl.handle.net/10986/31066 au direct link hii hapa https://openknowledge.worldbank.org...1066/9781464813863.pdf?sequence=8&isAllowed=y).

Ripoti ya World Bank inasema kwamba uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2018 ulikuwa kwa asilimia 6.0. Mwanzo wa ripoti imeandikwa kabisa kwamba “The cutoff date for the data used in this report was May 23, 2019.” Kwa hiyo kuna uwezekano wa kupishana kwa data. Ila bado kuna mkanganyiko kidogo. Ningetegemea “consultation” katika ya World Bank na NBS au Wizara ya Fedha kuhusu number hii muhimu na makubaliano kabla ya kuchapisha.
Naomba niishie hapo kwa jioni hii. Katika mada nyingine, uzi mwingine, na siku nyingine, nitaendelea na matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2019 and 2020 (mwaka wa uchaguzi).

Kwa muhtasari, maswali yangu ni haya hapa:

Moja: Kwa nini NBS wameacha kutoka ripoti za kila robo mwaka zenye kudadavua mwenendo wa ukuaji wa uchumi kutokea R2 2017 ili zifanyiwe kazi na wadau?

Pili: Kwa nini NBS hawajatoa ripoti iliyokamilika kuhusu ukuaji na mwenendo wa uchumi wa R1, R2, R3 na R4 ya mwaka 2018 kama ilivyokuwa miaka ya nyuma?

Tatu: Kwa mujibu wa taarifa rasmi, kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa mwaka mzima wa 2018 ni asilimia ngapi?

Nne: Kwa nini Zanzibar wameshafunga mahesabu yao ya pato la uchumi kwa mwaka 2018 na sisi huku bara bado tunasua?

Picha hii hapa chini inaonyesha hali halisi ya mkanganyiko wa taarifa kwa mwaka 2018. Pia, inaonyesha picha tofauti kabisa ya matarajio ya ukuaji wa uchumi wetu kwa mwaka 2019 and 2020. Hii nitaielezea baadae.

Wasalaam.
PSD.
Summary GDP Growth (Tanzania) - Copy.PNG
 
Angalia website ya BOT kuna annual report ambayo imetoka as of June 2018. Inaweza kukupa mwanga kidogo japo najua ulitaka kupata numbers za uchumi kwa tulivofunga mwaka 2018.

Tukubaliane na uhalisia kwamba nchi yetu ipo slow sana kutoa numbers za kiuchumi. Yaani gap inaweza kuwa hata miezi 12 wakati nchi za wenzetu mwishoni mwa kila quarter ya kwanza data za mwaka uliopita za kiuchumi lazima zitoke zote. Sijui tunakwama wap?
 
He he he, ina elekea una fanya kazi kwenye some international institution.

Traditionally ni mapema mno kupata takwimu za uchumi za the whole of 2018. Hususan detailed statistics. Na kwa takwimu nyingine za kiuchumi itabidi usubiri hadi 2020.

Na zikitoka usizifurahie sana, huenda zika over estimate mafanikio in some way.

Enjoy kuwa mtafiti kwenye nchi za dunia ya tatu.
 
Nchi ni masikini, so budget ya NBS ni ndogo.
 
Ni kweli hazijatoka au hujasikia..?

Tafuta mkuu..acha upapai..
 
Angalia website ya BOT kuna annual report ambayo imetoka as of June 2018. Inaweza kukupa mwanga kidogo japo najua ulitaka kupata numbers za uchumi kwa tulivofunga mwaka 2018.

Tukubaliane na uhalisia kwamba nchi yetu ipo slow sana kutoa numbers za kiuchumi. Yaani gap inaweza kuwa hata miezi 12 wakati nchi za wenzetu mwishoni mwa kila quarter ya kwanza data za mwaka uliopita za kiuchumi lazima zitoke zote. Sijui tunakwama wap?

Hii ripoti nilishaangalia mkuu. Haina takwimu za uchumi wetu kwa mwaka 2018.
 
He he he, ina elekea una fanya kazi kwenye some international institution.

Traditionally ni mapema mno kupata takwimu za uchumi za the whole of 2018. Hususan detailed statistics. Na kwa takwimu nyingine za kiuchumi itabidi usubiri hadi 2020.

Na zikitoka usizifurahie sana, huenda zika over estimate mafanikio in some way.

Enjoy kuwa mtafiti kwenye nchi za dunia ya tatu.

Hapana. Mimi niko hapa hapa bongo. Ila nimetokea kupenda kufanya utafiti wa kiuchumi. Takwimu ili ziwe na maana hazitakiwi kuchelewa!
 
Angalia website ya BOT kuna annual report ambayo imetoka as of June 2018. Inaweza kukupa mwanga kidogo japo najua ulitaka kupata numbers za uchumi kwa tulivofunga mwaka 2018.

Tukubaliane na uhalisia kwamba nchi yetu ipo slow sana kutoa numbers za kiuchumi. Yaani gap inaweza kuwa hata miezi 12 wakati nchi za wenzetu mwishoni mwa kila quarter ya kwanza data za mwaka uliopita za kiuchumi lazima zitoke zote. Sijui tunakwama wap?

Inasikitisha kwa sababu uchumi wetu ni mdogo. Kukusanya taarifa za uchumi mdogo ni rahisi zaidi. Angalia Marekani wameshatoa ukuaji wa uchumi kwa R1-2019. Pitia hapa https://www.bea.gov/news/2019/gross...second-estimate-corporate-profits-1st-quarter.

IMG_5764.JPG


NBS ina budget kubwa na pia inapata hela nyingi kutoka kwa wafadhili.
 
Hapana. Mimi niko hapa hapa bongo. Ila nimetokea kupenda kufanya utafiti wa kiuchumi. Takwimu ili ziwe na maana hazitakiwi kuchelewa!
Ok. Ila bongo si kuna matawi ya hizo international institutions.
 
Ok. Ila bongo si kuna matawi ya hizo international institutions.

Sifanyi kazi na hizi taasisi za nje. Niko katika kazi ya kawaida tu ya kuajiriwa ila nina passion na uchumi. Nilishaomba kazi Benki Kuu na kwengineko ila haikuwa rizki.
 
Sifanyi kazi na hizi taasisi za nje. Niko katika kazi ya kawaida tu ya kuajiriwa ila nina passion na uchumi. Nilishaomba kazi Benki Kuu na kwengineko ila haikuwa rizki.
PseudoDar186 uko vizuri! Poa kabisa. Unafaa kuwa mshauri was uchumi was Mkuu pale Magogoni. Nitakufanyia mpango. Serious!
 
Ccm wanaweza kukata mauno tu majukwaani
 
Nchi ni masikini, so budget ya NBS ni ndogo.
Wewe na mleta pambaneni na Hali zenu muondoe umaskini wenu binafsi mumekalia umbeya ohh TAKWIMU za umaskini wa nchi ninyi wenyewe choka mbaya.Pambaneni na umaskini wenu binafsi ambao hata TAKWIMU za umaskini wenu binafsi hamnazo.GDP ya majumbani kwenu ilikua kwa asilimia ngapi? Acheni umbeya
 
Wewe na mleta pambaneni na Hali zenu muondoe umaskini wenu binafsi mumekalia umbeya ohh TAKWIMU za umaskini wa nchi ninyi wenyewe choka mbaya.Pambaneni na umaskini wenu binafsi ambao hata TAKWIMU za umaskini wenu binafsi hamnazo.GDP ya majumbani kwenu ilikua kwa asilimia ngapi? Acheni umbeya
Takwimu za uchumi wa nchi ni muhimu sana kwenye kuondoa umaskini binafsi. Nitakupa mfano mdogo tu. Sekta ya ujenzi imekuwa kwa wastani wa asilimia 14.2 kati ya 2015 mpaka 2017. Kwa muda huo huo, sekta ya fedha na bima imetoka asilimia 11.3, 1.1 na mpaka kufikia -2.8 (yani imeporomoka kabisa). Hata ajira kwenye mabenki zimeshuka sana. Kwenye makampuni ya insurance ndio usiseme - mambo yamekauka mno na wengine walishafunga. Mdogo wangu nilimwambia mapema ahame kampuni mmoja mapema kabisa kabla ya mambo kuwa mabaya zaidi. Kwa kutumia akili ya kawaida, bora nikaombe kazi kwenye ujenzi ambao unakua kwa asilimia 14.2 kuliko kubaki kwenye sekta inayoporomoka! Ni kujiongeza tu. Hizi data muhimu sana!
 
Ni kweli hazijatoka au hujasikia..?

Tafuta mkuu..acha upapai..

Acha kujibu tu kwa sababu waweza kutype.

Mleta mada kakupa links...kukuonesha alivyotafuta kujua.

Sema "they are all Greeks to you"
 
Acha kujibu tu kwa sababu waweza kutype.

Mleta mada kakupa links...kukuonesha alivyotafuta kujua.

Sema "they are all Greeks to you"
Ukweli ni kwamba, tuko katika giza kuhusu uchumi wetu kwa mwaka 2018 na 2019 (robo ya kwanza). NBS inabidi watoe takwimu ili tuweze kufanya udadavuzi tujue tunaelekea wapi.
 
Back
Top Bottom