Kwanini TAMISEMI haitoi hela ya usimamizi wa miradi yake?

Kwanini TAMISEMI haitoi hela ya usimamizi wa miradi yake?

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Sote tunashuhudia mabilioni ya fedha za miradi ya TAMISEMI kwenye Halmashauri kadhaa hapa nchini. Ni hatua kubwa sana kwa maendeleo ya nchi.

Tuna miradi ya shule, mabweni, vituo vya afya, Hospitali, nyumba za watumishi, majengo ya utawala n.k n.k

Unakuta TAMISEMI Makao Makuu wanaleta fedha mfano Milioni 250 za vituo vya afya lakini hawaleti fedha za usimamizi wa kazi. Kitendo cha kuziachia Halmashauri jukumu la kuwawezesha wataalamu kusimamia miradi hiyo siyo jambo jema, kwani hazina uwezo na inajulikana hivyo.

Badala yake mafundi wanajenga miradi bila uwepo wa wataalamu (full supervision) hata mshauri mwelekezi.

Kazi hazina ubora unaotakiwa. Kazi ni mbovu sana.

Ni jambo la kufikirisha sana TAMISEMI kutoa Milioni 250 ya kazi bila hata 10m ya usimamizi wa kazi

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hizi kazi za hovyo hovyo za akina Ummy Mwalimu na Mwigulu Nchemba za Force Accounts zitakuja kuligharimu sana Taifa hili!

Tumesomesha vijana wengi Civil Engineering na wamesajili kampuni zao CRB na hawana kazi wamekaa mtaani!

Anakuja mtu mwenye maarifa madogo eti hakuna cha mkandarasi kupewa kazi bali mafundi uchwara wa mtaani (local fundis)

Hivi ma QS na Ma Engineers wanaoandaa BOQ za miradi katika maeneo hayo wana kazi gani mpaka muogope eti kuibiwa na Wakandarasi? Tuna viongozi myopic sana na wanaleta sera za hovyo kabisa!

Ngoja mjengewe miradi ya hovyo kwani hata mawazo yenu ni ya hovyo kabisa!

What goes around comes around!
 
kufanya kazi na kampuni za wabongo ni sawa tu na kufanya na mafundi uchwara, yaani kampuni ya kibongo ikipata kazi wanawaza nani wa kula nae kuliko kazi kuwa bora matokeo yatakua ni kazi mbovu tu. Anyway kabla ya kujali kampuni za ndani wajitathmini kwa kufanya kazi bora 🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Wewe utakuwa mtumishi wa Serikali ( Posho team)! Nataka nikuambie Kampuni nyingi za Wabongo zinafanyakazi nzuri sana isipokuwa nyie ving'ang'anizi wa 10% mlioko Serikalini ndo mnawaangusha.

Mnataka rushwa kuanzia mchakato wa kumpata Mkandarasi hadi wakati wa malipo.Sasa unadhani mkandarasi atafanya nini ni lazima achakachue kazi vinginevyo anawafanyia nyie kazi!

kufanya kazi na kampuni za wabongo ni sawa tu na kufanya na mafundi uchwara.....yaani kampuni ya kibongo ikipata kazi wanawaza nani wa kula nae kuliko kazi kuwa bora ..matokeo yatakua ni kazi mbovu tu ....anyway kabla ya kujali kampuni za ndani wajitathmini kwa kufanya kazi bora...🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Back
Top Bottom