Kwanini Tanasha hakubaliki kwa Diamond Platnumz?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Na Mpenzi wake Tanasha Donna.

JARIBIO halipo mbali. Halichukui muda mrefu sana kutoa majibu. Cha kufanya, chukua picha kali ya mrembo Tanasha Donna. Hakikisha ina mvuto wa kutosha. Usiandike neno lolote la kuonesha upo upande gani kisha weka picha hiyo kwenye ukurasa wa mtandao wowote wa kijamii kama Twitter, Facebook, Instagram au WhatsApp.



Dakika kadhaa baadaye, fungua sehemu ya “comments” (maoni), utakutana na majibu juu ya kwa nini mashabiki lukuki wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ hawamkubali mchumba’ke wa sasa, Tanasha Donna Oketch.



Tanasha ni mtangazaji mrembo kutoka nchi jirani ya Kenya. Ana takriban miezi mitatu tangu aingie kwenye uhusiano wa kimapenzi na Diamond ambaye ni mwanamuziki wa kimataifa anayepeperusha vyema bendera ya Bongo Fleva.



Katikati ya mapenzi motomoto baina ya wawili hao huku jamaa akimmwagia sifa kedekede, baadhi ya mashabiki wa Diamond au Mondi wameendelea kuwa vichwa ngumu. Hawakubali kusikia Diamond anamuoa Tanasha. Ndiyo maana wakati Diamond anatangaza kuahirisha zoezi la kufunga ndoa na Tanasha lililopangwa kufanya Februari 14 (Valentine’s Day), mwaka huu, kuna watu walichekelea meno thelathini na mbili yote nje.

Walio upande wa Tanasha wameendelea kubaki wachache. Mbali na Mondi ambaye hilo ndilo chagua lake ambalo upende usipende anasikiliza matakwa ya moyo wake, wengine ni mama yake, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na dada’ke, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.



Dada yake mwingine, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ hana habari na Tanasha, yeye bado anamuota Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni ‘eksi’ wa Mondi aliyezaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan. Watu kama kaka’ke, Rommy Jones huwa wanafuata tu anavyotaka Mondi.


Wengine ni waja ambao kazi yao ni kudandia ishu za watu. Hawa hata kama Mondi angesema anamuoa msichana asiyejulikana huko Tandale-Magharibi wangeshadadia na kumsifia. Mfano wao niJuma Lokole. Lakini kwa nini baadhi ya watu hawamkubali Tanasha? Uchunguzi wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko una majibu;



VIATU VYA ZARI HAVIVALIKI

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, bado wasifu wa Zari ni maji marefu kwa Tanasha. Wapo wanaokiri kuwa viatu vya Zari havivaliki kirahisi. Ama vinambana au kumpwaya Tanasha. Wengi wanasema kuwa Zari ni mama bora kwani ni mama wa watoto watano, lakini amekuwa mfano bora kimalezi, kipimo ambacho kwa Tanasha hakipo.


MVUTO WA NJE

Achana na mambo ya kuwa mama bora, lakini vipimo vya nje vinaonesha kwamba wapo ‘ma-ex’ wa Diamond wanamzidi Tanasha ambaye hafi kii kiwango chao cha mvuto wa kimaumbile. Pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka 23, lakini hafui dafu kwa Zari anayegonga umri wa miaka 40 au Wema mwenye 30. Mfano unaotumika ni ‘kifua’ chake kulegea mapema kabla hata ya kunyonyesha.



NYOTA

Ipo ishu inayozungumzwa zaidi ya nyota. Wakati Mondi akiwa na kina Wema Isaac Sepetu au Zari, nyota yake iling’aa mno. Wapo wengi ambao wanaamini kwamba nyota ya Tanasha imepoa ukilinganisha na Wema, Zari na hata Hamisa Mobeto.

NGUVU YA MA-EX WENGINE

Ukweli mwingine mchungu ni kwamba Tanasha anazidiwa na wingi wa wafuasi wa ma-ex wa Mondi. Kwa haraka haraka ukitazama kwenye kurasa zao za Instagram, Tanasha ana wafuasi kiduchu ambao ni laki 3.5 ukilinga nisha na Zari mwenye wafuasi milioni 4.9, Wema milioni 4.5 na Mobeto milioni 3.3 hivyo nguvu ya umma ndiyo inayoongea!
 
Zari alikuwa na followers wasiozidi laki 2 kabla ya kuwa na diamond,baada ya kuwa na diamond ndio kapiga jackpot!
Hata Tanasha atagonga followers kibao in a short while
 
Okky.

Tumekupata mkuu. Endelea kutuhabarisha ukipata ubuyu mwngne
 
Pamoja Na uzuri wa Mtu unategemea Mtu lakin kwa mtazamo wangu Huyu Binti ni wa kawaida sio Yule wa kuleta 'Heart attack'

Kwanza Ana kitumbo sifa ambayo kwangu Ni Kama Kupata F ya hesabu Kwenye NECTA ya Form four Yaan Hata Kama una Div 1 unashushwa kwenye three Kama Penalt

Pia hana sura ya Kibashasha Yaan ile sura ya 'kufungua Mwamvuli' Hata Kama Hakuna dalili ya Mvua

Kapewa weupe tu Mengine Hata 'Mwazani wa Biti Jongo' anavyo
 
Unaweza kushangaa hii mada kaleta mwanaume. Naombeni wanaume mbadilike msiwaige Dada zetu mambo ya umbea hiyo ni furaha yao wao.inatakiwa tujadili mambo ya maana kidogo,afadhali ungeleta mwenendo wa msanii mwenyewe kwenye bongo fleva , sahv Nigeria wanazidi kitupiga gape kwenye mziki kutokana hadi wanaume wa Tanzania wanaendekeza umbea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aaah zari bana asirudi madale labda kama atarudi kwa nia ya kumkomoa mama dai ila pale hapamfai kwa sasa alee tu wanae
Shangaaa, aache kuwa na mtoto mbichi eti akaparamiane na Wema au mama wa dua[emoji16]...

Kidogo Zari ndo ana ubavu coz tayari wana family...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nahisi kama tatizo ni diamond. Kwa sasa watu wanamuangalia tu maana ni kitombile. Atajitia mahaba ya kushikana na sifa nyiingiii. Baadae wanabwagana. Kiki kwake ya wanawake kama inapungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…