Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wiki kadhaa zilizopita TANESCO walikuja kwangu kubadili mita (niliwaita kutengeneza kutokana na mita kuwa inajizima yenyewe, walipoitazama wakasema lazima iwekwe mpya) hivyo wakasema watakuja watu wataoweka hiyo mita.
Kesho yake mapema wakaja watu wengine kuniwekea mita, wakaangalia umeme uliopo Wakakuta nina unit nyingi, wakasema inabidi tusibadili maana una umeme mwingi na tukiweka nyingine hautaupata na kama ukiupata utakuwa umeteseka vya kutosha na utatumia muda mrefu mpaka uje kupata huo umeme.
Wakasema nitumie zikibaki unit kuanzia chache wakanitajia kiwango niwaambie waje, mmoja wao akaniachia namba kuwa nitapiga kuwajulisha, zilipobaki hizo walizosema nikawajulisha wakaja, Walipokuja wakasema mita wanayoweka ina unit kidogo na hizo unit nitatakiwa kuzilipa kila nikiweka umeme watakata 3000, nikawauliza vipi kuhusu hizi unit zangu chache mnazozichukua wakasema fanya kusamehe maana kuzipata ni mchakato mrefu na zitakutoa jasho.
Nikaongea katika utani kuwa siyo kwamba ndio inakuwa fidia maana zimelingana na mnazonipa hapa wakasema hapana hizo fanya tu kusamehe.
Nilichogundua wao wamejiwekea utaratibu wa kurudisha zao wanazokupa wakibadili ila hawana utaratibu mzuri wa kurejesha wanazochukua, na wanasumbua mpaka uziache.
Pia soma: