Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Nchi nyingi, hasa zile zinazozalisha dhahabu huwa zinachapisha sarafu za dhahabu na kuuza. Sarafu hizi zina mambo mengi. Kwanza watu hununua kama kito kutokana na uzuri wake.
Pili watu hununua kama ni pesa na wanaweza kuitumia kama pesa. Tatu nchi hufanya export ya kitu kilichoongezwa thamani na kujipatia pesa.
Nne zinatumika kutangaza mambo ya nchi, hasa utalii. Tano na muhimu zaidi, watu hununua ili kulinda utajiri wao dhidi ya mfumuko wa bei.
Nchi nyingi hutengeneza sarafu hizi zikiwa na uzito wa ounce(oz) moja ambayo ni sawa na 31g. Ikiwa ni 99.99 pure gold. Bei ya oz moja ya dhahabu kama hiyo kwa sasa ni dola 1,900. Wanatengeneza pia sarafu zenye uzito wa chini.
Nchi kama Rwanda wanatengeneza sarafu zao za dhahabu toka 2018. Na wakongwe wa hizo kazi ni SA, USA, Australia, Canada na Austria. Hizi sarafu zinafaida nyingi kama tulivyoona, na nchi yetu ina dhahabu ya kutosha. Na sasa tunazo refineries. Kwa nini hatutengenezi hizi coins, labda serengeti, ngorongoro, kilimanjaro etc, na kuwauzia raia na wageni pia?