Kuwa na app store hauitaji kuwa na mfumo wa OS yako hasa upande wa android.
Zipo app market place nyingi tu ambazo hazimiliki operating system ya android ama kumilikiwa na google.
Kwa mfano iran kuna android app store yao inaitwa
Cafe Bazar ambayo ni maarufu kule ikiwa na watumiaji 40m, imelenga developers na wateja wa iran.
Mwanzilishi wa hiyo app store hana operating system bali ni android app market place kwa ajili ya watu wa iran.
Lakini kuna apps stores zingine kama palmstore, amazon appstore, QooApp n.k
Tukija kwenye swali.
Kutengeneza app store kwa ajili ya tz sio ishu kiasi hicho iwapo una server yenye uwezo mkubwa wa kuhandle request nyingi(hii ndio challenge kubwa)
Pili na utayari wa watanzania kulipokea hilo soko la app za kitanzania kwa sababu ni upotezaji wa muda na pesa iwapo hakuna watu watakapakua app kutumia hiyo store.
Lakini sio tu kuwa na watumiaji, watumiaji ambao wako tayari kutoa hela kwa ajili ya huduma zinazotolewa na apps?
Watanzania wengi hawapendi kulipia hivyo vitu wengi wapo tayari kutumia pirated apps iwapo app ni za kulipia.
Kama app ni ya bure na ikawa na matangazo watz wengi huchukia na kuamua kuweka ads blockers.
Na hapo utapaswa kuzi-cover gharama za uwendeshaji kuanzia servers, waajaliwa(software developers), promotion budget, kodi za serikalini nk.
Ukichunguza utagundua gharama zitakuwa kubwa hivyo utahitaji ku-raise funds.
Sasa kama kuna investor anaweza take risk kwenye nchi ambayo inaweza ikafunga internet kwa karibu wiki mbili basi itakuwa njema.