Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Kwenye computer 🖥️ ikiingia virus🦠🦠 unatakiwa upige chini ⬇️ windows utoe uchafu wote uanze upya...hata huku ilitakiwa iwe hivyo hivyo....ilitakiwa raia wote wapigwe chini 💣🔫waje binadamu kutoka pande nyingine za dunia waanzishe maisha mapya
 
Furaha itatoka wapi wakati wewe hata kiwanja kisiju huna ..........mwenzanko mtoto wa kigogo ananunua morroco square apartment na tena wala hana muda wa kuishi wala kuipangisha ipo tu ............
😅😅
 
Kwenye computer ikiingia virus unatakiwa upige chini windows utoe uchafu wote uanze upya...hata huku ilitakiwa iwe hivyo hivyo....ilitakiwa raia wote wapigwe chini waje binadamu kutoka pande nyingine za dunia waanzishe maisha mapya
Wanasema hata kama wazungu wakija Afrika na waafrika wakaenda uzunguni baada ya miaka kumi tu, afrika itajengeka kama uzunguni na uzunguni patakuwa kama Afrika!
 
huku kwetu hayo yamebakia kuwa hadithi hadithi uongo na utamu kolea, ni ndoto tena ya mchana! Tumeishia kuyaona kwenye TV.
 
Kuna watu walikuwa wanachangia mjadala kwenye blog moja. Lilian Mwasha alikuwa anahojiwa kuhusu usafiri wa daladala. Sasa wameweka kipande tu cha video akisema hawezi panda daladala hata iweje. Ee bwana wee, watu wametokwa mapovu, sijui kwani yeye ana miadi na Mungu, asijitie kiburi na mengine mengi. Yaani unaona watu wana wivu wa kijinga kabisa.
Chuki zimewajaa sababu hawana furaha.
 
Nchi kama Finland muda mwingi ni baridi hawawezi kuzalisha chakula lakini wamewekeza kwenye mambo mengine ya kuwaingizia kipato.
 
Lazima wawe na wivu maana ni kama tamthilia fulani hivi hawajawahi kuishi maisha hayo, hata mtu humu akisema hali ugali anakula diet ya maana, mashambulizi yatakua mengi mara unajiona mara hivi mara vile!
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!


Mama Samia na familia yake , Kikwete na familia yake na vigogo wa CCM wana furaha sana. Machawa watakuja hapa na kukubishia kwasababu wenyewe binafsi wana furaha sana na pesa za uchawa za Mama huku Watanzania wengi wakiwa hawana furaha wala matumaini.

Sasa utafurahi vipi wakati kijana huna kazi, kura zinaibiwa, hakuna hata wasemaji kura ni fake za polisi na usalama , wapinzani wanaokupigania basi ndiyo wanatekwa na kupigwa risasi. mikataba basi iwe ya wazi hapana ni ya siri na wanawekewa pesa huko nchi za waarabu. Vijana wenye pesa ni watoto wa Samia , kikwete , Pinda na viongozi wengine. Vijana wetu wamekuwa machawa hata hapa tunao! furaha itatoka wapi!

ChoiceVariable

Pascal Mayalla
 
Hamwezi kuwa na furaha kama huduma za msingi kila mahali ni mbovu na hadi utoe rushwa ndo shauri lako lifanyiwe kazi.
Hamwezi kuwa na furaha kama watoa huduma ni watu wasiojali. Kwa mfano mzee ambaye ni mwanachama wa PSSSF amekuwa akichangia sasa kastaafu lakini kuja kupata mafao yake hadi azungushwe na bado akutane na kikokotoo.
 
Kamundu hali inatisha kesi za kujiua zinazidi kuwa nyingi!

Ajira zinazidi kuwa adimu.

Tsh inazidi kufa thamani dhidi ya dola $.

Deni lataifa ndio hilo linaenda $100T.

Umeme waliahidi watauza mpaka nje ila sasa wananunua kukidhi uhaba kanda ya kaskazini!
 
Samia ndio amekunyima kazi? Ndio alikuzaa? 🤣🤣

Yule shujaa wenu Kwa nini hakuwapa kazi ? Wakati anaharibj uchumi si mlisema anainyoosha Nchi? Saizi ananyooka nani? 😆😆
 
Mashamba yameisha?
 
Hao wote sio Watanzania wanaofanya Bali ni Waarabu au siyo? 🤣🤣
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Unatakiwa kujisemea mwenyewe usijumuishe.

Harafu kuna watu wanaodai hakuna Ajira,huku nilikp Niko natoa Ajira ila Vijana hawataki wanadai hela ndogo kazi kubwa Bora wawe kijiweni 🤣🤣

Watu wa hivyo hata wakifa njaa ni kufikia tuu
 

ChoiceVariable machawa mtashangaa sana tunasingiziwa eee!! Huu ni uongo eti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…