Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Dah inasikitisha sana, ila kuna nchi zinapitia majanga kama ukame na vita zisizokoma mfano Somalia, nilitegemda amani inayosifika Tanzania iendane na furaha!
Kwa porojo za ccm Tanzania ni nchi ya amani, lakini kiuhalisia unaofahamika duniani ni nchi ya majoga na sio amani.
 
Vipi huko umeme wa Ethiopia mmeshaanza kutumia au bado haujafika hapo?
 
Unalima wapi kwanza, unalima kwa pembejeo zipi? hata ukifanikiwa unauza wapi? hata ukiuza mda wa kuuza bei unapangiwa! wanadai kilimo ni uti wa mgongo ila mkulima serikali haimjali mkulima anachukuliwa kama mtu aliefeli maisha.
Kweli kabisa, hadi kulima inatumika kama kejeli. Nadhani umewahi kusikia kama maisha yamekushinda hapa mjini, rudi kijijini ukalime.
 
Unamsikiliza mtu anadanganya, unaona kabisa kuwa huyu anadanganya, na yeye mwenyewe anajua anadanganya, lakini anadanganya mpaka hata yeye mwenyewe anaanza kuuamini uongo wake mwenyewe...
hahaha dah kwamba unajua unadanganywa ila unakubali mpaka uongo unauona ni ukweli.

Umenikumbusha siku moja nilihisi njaa mpaka njaa ikazidi nikahisi kushiba 🙂
 
Kweli kabisa, hadi kulima inatumika kama kejeli. Nadhani umewahi kusikia kama maisha yamekushinda hapa mjini, rudi kijijini ukalime.
Sahihi mkuu, na kama kuna watu wanaochukuliwa wamefeli maisha ni mwalimu na mkulima.
 
Unalima wapi kwanza, unalima kwa pembejeo zipi? hata ukifanikiwa unauza wapi? hata ukiuza mda wa kuuza bei unapangiwa! wanadai kilimo ni uti wa mgongo ila mkulima serikali haimjali mkulima anachukuliwa kama mtu aliefeli maisha.
Unaongea kama vile hayo hayafanyiki.

Tafuta sayari Yako ndio utaamua Kila kitu mwenyewe
 
Natumaini ni kwema wakuu.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya orodha ya nchi zenye furaha duniani, Tanzania(136) tumepitwa mpaka na Somalia(122).

Imesikitisha sana hii habari ni kana kwamba naishi nchi ya majonzi,huzuni, na masononeko!
Weka source
 
Nchi kama Finland muda mwingi ni baridi hawawezi kuzalisha chakula lakini wamewekeza kwenye mambo mengine ya kuwaingizia kipato.
Safi kabisa. Je, hapo umeiona siasa? Kama jibu ni hapana,ni kwa nini basi nasi waTz tusifanye hivyo? i.e. Tuwekeze kwenye mambo mengine ya kutuingizia kipato - kuanzia ngazi ya Familia hadi ngazi ya Taifa (Nchi)kama wanavyofanya Finaland? Tunakwama wapi ilhali Wataalam wapo tele.
 
Nanukuu: "Mavijana ya kitanzania HOVYO KABISA! kazi umbea na majungu tu"
Kweli. Kutwa nzima ni unywaji wa energy iliyochanganywa na kisungura au Jogoo; halafu ni makelele ya Ubishi wa Simba na Yanga. Halafu kiuchumi hali inapozidi kuwa mbaya lawama zinaelekezwa kwa CCM kana kwamba CCM ndo wameshikilia Fursa zao. Siwatetei CCM lakini Ukweli usemwe. Kama kuna kijana alikuwa anajitafuta halafu CCM ndo ikaja kumkoroga mahesabu yake aseme hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…