Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Kaitafute inakopatikana.Harafu jisemee wewe usijumuishe watu wote kwenye swala Hilo la furaha.
Hii 👆 👆 haijakaa vizuri. Mtoa mada amesema waTz (kama sijakosea )hawana furaha. Hakuna alipoandika au kusema waTz wote. Hata kwenye Ranking iliyowekwa, waTz wameshika namba 136 manake orodha hiyo inaendelea 137, 138, 139 n.k. i.e. waTz sio tumeshika mkia-Hapana. Wapo tuliowazidi kwenye kinyang'anyiro hicho cha Furaha.
 
Kwani toka viongozi wetu wa kiserikali waanze kututapeli, tulishtuka lini, mara viwanda kubinafsishwa, mara ununuzi wa rada, epa na richmond, mara bandari, sijui wanyama, ripoti ya CAG kila siku ina madudu lakini tupo kimya tu.
Uzezeta pro max!
 
Ila hata nchi zilizoongoka kwenye orodha mfano Finland pana maovu pia kama ndoa za jinsia moja ,uhalalishwaji wa kutoa mimba n.k
 
Trump ana miaka mingapi amechaguliwa Rais wa Marekani? Hiyo siyo sababu, Wasira kuteuliwa makamu m/kiti inakunyimana furaha? Shida anayepima hicho kiwango cha furaha ndiyo hao wamejiweka nafasi za juu kuwa wana furaha. Wazungu wanatuchezea tu akili, we fanya mambo yako acha kuwaza wenzako furaha utajipa mwenyewe
 
Siasa ipo sana. Kuna demokrasia na uhuru wa kweli. Uchaguzi huru na wa haki. Kiongozi akishindwa kufilisha malengo aliojiwekea anajiuzulu. Serikali ya sasa ni ya mseto. Vyama zaidi ya vi 2 vinaendesha Serikali.
 
Ila hata nchi zilizoongoka kwenye orodha mfano Finland pana maovu pia kama ndoa za jinsia moja ,uhalalishwaji wa kutoa mimba n.k
Wana maovu lakini si ya kudhuru mtu mwingine. Uwe shoga ni chaguo lako ,lakini ushoga wako usiwe bughdha kwa watu wengine. Maovu mengi ya Tanzania ni ya kudhuru watu wengine
 
Sasa anatarajia kuipatia furaha kwenye matusi kweli jamani, humkini anamsongo.
Huenda maana tatizo la afya nchini ni kubwa, furaha inatafutwa kwa njia zisizo za kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…