Kwanini Tanzania hatuna furaha? Nini kifanyike?

Ni kigezo gani au ni kipimo gani kimetumika kubainisha uwepo wa hiyo Furaha?
-Huduma bora za maji,umeme,afya. Je wananchi wanaridhika nazo?
-Utawala. Wananchi wanaukubali kwa kiasi gani?
-Mazingira na hewa safi.
-Usawa wa kibinadamu na kijinsia na nyinginezo...
 
Uongo barani Afrika upo na utaendelea kuwepo maana hatutaki kubadilika. Plus unafiki mwingi na sasa umekuja uchawa.
 
Kodi zinatolewa na wananchi ila wajanja wanafaidi, ni huzuni kuwa na mtaro mchafu unaosambaza magonjwa na kodi zinatolewa. Ni huzuni kuona waziri anapanda ndege daraja la kwanza kwenda kusaini mkataba fake huko nje. Kila kitu ni huzuni, huzuni kusikia mdogo anakaripiwa "unanijua mimi ni nani?" Ili huzuni ipungue tunahitaji viongozi wazalendo na wenye maono. JPM alituletea raha ila kwa mda mfupi RIP.
 
Inchi inayoongozwa na kiongozi mkuu asiye na uwezo(incompetent), aliyepata nafasi hiyo kwa ngekewa tu unategemea tuwe na furaha?
Ni mwaka muafaka wa kutafuta competent leader.
 
Kuhusu kwenda veta ni personal issue
Uko sahihi Red black tatizo kauli ilitolewa na mwanasiasa baada ya walimu kucharuka. Pia ukienda SIDO kuna masomo mengi tu ya ujasiriamali kwa vitendo. Tatizo wanaleta siasa kwenye mambo ya msingi. Wako wasomi wengi tu wamejiongeza, wako wanaoendesha bajaji na boda boda pia. Tatizo ni siasa inapotumika kutatua tatizo la kiufundi.
 
1. Vikoba
2. Kausha damu
3. Usaliti
4. Ccm
5. Ajira
6. Kamari
7. Uraibu

Huwezi pata furaha, kwa kila mtanzania Kimoja kati ya hivyo kinamsumbua
sina kinachonisumbua kwa hiyo orodha ya kero, na CCM ni mkombozi wangu, I am happy always, rember the World is Living SUFFERING is your CHOICE
 
Kwa Tanzania mechi Kati ya Simba na Yanga afu timu moja ipate ushindi bila Shaka kuna watanzania lazima watakuwa na furaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…