Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Footballers with degrees: Kompany, Mata & 10 players who went to university | Goal.com

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Eti ndugu zangu watanzania;

Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Chila Tenga pamoja na ndugu Mohamed Mbwana Bakari "Junior"? Tunakwama wapi kama taifa?

Ninasikia huyu Mbwana Mohammed Bakari "Junior" alikuja kuwa boss mkuu (Commissioner General) wa idara ya uhamiaji hapa nchini baada ya kuacha kucheza soccer.

Ukijaribu kuangalia kwa haraka haraka katika kikosi cha timu ya taifa ya Soccer ya Tanzania (Taifa Stars) utakuta mchezaji mwenye elimu ya juu ni form six tu.

Kwanini vilabu vya soccer/michezo hapa kwetu havitoi msisitizo kwa wachezaji wao kujiendeleza kielimu ilhali inajulikana fika ya kuwa mchezaji hata kama akiwa ni tajiri sana akisoma anakuwa katika nafasi nzuri ya kusimamia vema mali zake?

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya mdau
 
Infantry Soldier,

KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.[/QUOTE]Nafikiri ni mifumo ya upatikanaji wa hao wachezaji kubadilika...Mathalani mashindano kama Umitashumta na Umiseta hayatoi vipaji vyenye muendelezo(kielimu na kimichezo) lakini pia Serikali kupitia taasisi zake/wizara hazina sera au Watekeleza Sera madhubuti.
 
Nafikiri ni mifumo ya upatikanaji wa hao wachezaji kubadilika...Mathalani mashindano kama Umitashumta na Umiseta
Mkuu, kwani hao wanafunzi wanaoenda huko UMITASHUMTA na UMISETA si ndio hao hao ambao wapo huku mtaani wanacheza ndondo cup na kuonwa na TFF?

Tatizo ni serikali au ni wanafunzi wenyewe?
 
Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Chila Tenga pamoja na ndugu Mohamed Mbwana Bakari "Junior"? Tunakwama wapi kama taifa?
Kwani walisoma wakati wanacheza mpira, au baada ya kustaafu soka?
 
uliowataja ni wachezaji wa kawaida ..una miaka 19 unalipwa $200,000 kwa wiki acha masihara
Sasa mkuu, hauoni kuwa mchezaji tajiri akisoma anakuwa katika nafasi nzuri sana ya kusimamia vema mali zake?
 
Huyo tenga na mbwana ilitokea tu kama kunguru kumnyea binaadamu. si kana kwamba eti enzi hizo kulikuwa na vipanga kunako soka. Na ili kulithibitisha hili ebu nitajie graduate wengine japo watatu mbali na hao wawili! Siku zote mpira wake maselaπŸ˜€ haruna moshi,kelvin yondani,juma nyoso etc.
 
Mbali na mata na huyo kompany hao wengine wakuokoteza labda Socrates. Mpira wake masela mkuu. Ikitokea graduate ujue hiyo kunguru kumnyea binaadamu
Sasa mzee baba, hauoni kuwa mchezaji tajiri akisoma anakuwa katika nafasi nzuri sana ya kusimamia vema mali zake?
 
Nyumbani ukiacha shule ucheze mpira ni kipigo, shule ukitega kisa kuna mechi mtaani ukibainika kipigo... ukijigawa huku na huku basi unakuwa average tu kila sehemu!
 
Sawa mmakonde Infantry Soldier. Ngoja wataalam waje watakujuza zaidi. Vp NSSF walikupa pesa zako au ndio classified information?πŸ˜ŽπŸ˜ŽπŸ˜›
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…