Kwanini Tanzania inashindwa kuzalisha tena wachezaji ambao ni "University Graduates" kama akina Engineer Leodgar Tenga? Tunakwama wapi kama taifa?

Ume uliza kitu kizuri maana nasikiaga hiki kinacho tokea uganda leo walikujaga kuiga Tanzania miaka ya zaman ndio maana leo pale Uganda uona mchezaji kama Lwanda ni Engineer na anaupiga mpira wa kutisha ila Tz tuna wachezaj tulio waibua vijiweni ndondo
 
Tenga kasoma alivyoacha mpira, Mayai kasoma akaacha mpira, hakuna msomi Tanzania ambae alimaliza university akaendelea kucheza mpira tusidanganyane
 
Messi na Ronaldo wana degree ngap?....mashabiki wa insta tuacheni na mchezo wetu pendwa...Tenga na huyo mwingine uliomtaja walicheza mpira wa amateur ....Ajibu darasa la saba ana nyumba mbili za maana mjini
Hivi unaweza mlinganisha Ajib na Tenga?

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Tenga kasoma alivyoacha mpira, Mayai kasoma akaacha mpira, hakuna msomi Tanzania ambae alimaliza university akaendelea kucheza mpira tusidanganyane
Nilipokuwa benki kuu (BoT) kurugenzi ya utafiti na sera za uchumi niliambiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa kurugenzi hiyo Dr. Joe Masawe kipindi hicho kuwa kuna mtu alikuwa anaitwa Mwalusako kama sikosei aliwahi kufanya kazi hapo, aliacha kucheza mpira akiwa Yanga miaka ya 90 mwanzoni akajiunga na benki kuu kama mchumi daraja la pili tayari akiwa na shahada ya Kwanza na ya pili ktk uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 
Ulipiga kazi BOT? Upo vizuri sana mzee baba
 
Ulipiga kazi BOT? Upo vizuri sana mzee baba
Kwani nini Jombaa? Nilikuwa nanyoosha maelezo hapo juu ya mtu aliyekuwa anacheza mpira wa ushindani ngazi ya juu kabisa ( super league) huku akifanya full-time programme chuo kikuu hapa hapa Tanzania.
 
Mishahara ya BOT ni mireeefu sijapata kuona jombaa
 
Mishahara ya BOT ni mireeefu sijapata kuona jombaa
Sio kweli Jombaa, ni propaganda tu. Inafanana sana na ile ya wahadhiri vyuoni.

Junior/Entry Level vs Tutorial Assistant to Principal Level vs Senior Lecturer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…