Nyie bwana hamaishi maneno, jana nilikuwa nasikiliza wimbo mmoja eti "..TANU ilipoanza mwingereza kafunga vilago". Eti kuna watu wanaamini kuwa wakoloni walifukuzwa na TANU wakati wenyewe ndio walikuja hapa na baada ya miaka kama 30 wakampata kijana wakampeleka kumsomesha huko huko kwao na kumfundisha walichotaka wao ili baadae wamkabidhi nchi!
Wakoloni walikuja kipindi kimoja Afrika nzima na waliondoka almost miaka inatofanana, 1960s, hii haikutokea kwa bahati mbaya bali inawezekekana walikuwa na mpango wa labda miaka 300. Sasa jiulize mpaka leo bado mingapi imebaki wakati mkuu Trump anasema tunapaswa kuongezewa mingine 100!
Haya leo wameshaondoka, nenda Geita ukachimbe hiyo dhahabu tuone kama utaweza. Na hata ukiamua kuwekeza hazina yako yote kununua hizo mashine bado wenyewe ndio wanunuzi wa hiyo dhahabu, wakikataa kuinunua hata ukiwa na tani mia unakufa nazo na njaa! Hapo ndipo huwa tunasema life is not fair!