Kwanini Tanzania kwenye mahafali wageni waalikwa sio watu waliofanikiwa bali watu wa siasa/watu wa Serikali tu?

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu Habari zenu?

Kuna kitu hapa kwa wageni wahalikwa kwenye mahafali ya wanafunzi wa kumaliza chuo kikuu au shule hizi za secondary. Hivi ni kwa nini wasialikwe watu waliofanikiwa kimaisha ili waongee na wanafunzi hao na badala yake mnawaalika wanasiasa na wakuu wa mikoa kuja kutoa hotuba hapo kimsingi hawana chochote cha maana chakujifunza kutoka kwao?

Inamaana hakuna watu waliofanikiwa kwenye nchi yetu wanaweza kuongea na wanafunzi wetu? Sasa sijajua wanawaalika hao wanasiasa sana ili sijui wakielezea na shida zao waweze kusaidiwa lakini mbona muda mwingine hawatoi chochote wanatuachia maneno ambayo hata yeye mwenyewe bado anajitafuta kwenye game.

Leta watu waliofanikiwa kwenye lolote lile halafu kupitia kufanikiwa kwake anatufundisha kuzingani vitu gani na sisi tunaotoka chuo/mashuleni tuzingatie hiyo vitu japo kwa uchache tu.hapo inakuwa rahisi kukumbuka .

Nasio kusikia historia ya Maisha ya mtu aliyefanikiwa kwenye mahojiano ya vipindi vya television tu na kusema nchi hii watu historia zao hawaweki wazi, wakaweke wazi wapi sasa?

Mfano Samatta au millardayo(unaweza kuchagua na wewe wa kwako wengine ), hata nawafanya biashara, watu wengine kwenye kila sehemu walishakuwaga the best au sasa hivi ni bora wahalikwe waje waelezee wakonnect mafanikio yao na ushauri wao kwako wewe wanafunzi unaenda kupambana uraiani atleast tungepata kitu na tungekuwa tunatunza kumbukumbu na sio hao wanasiasa na wakuu wa mikoa ndio watoa risara na baada ya hapo hakuna cha maana anasubiria kuteuliwa tu.

Naishiaga tu kuwaonaga kwenye list ya influencer 100 Tanzania Fulani yupo bhana, sasa hao watu wengi wao wanakuwa wamefanikiwa kwenye kitu Fulani yapo sio kivile, ila ndio watu tulionao kwa sasa, na sio kualika watu wa hovyo hawana msaada wowote kwa wanafunzi, bali chuo/shule.

Shule /chuo inaalika mgeni rasmi kwa wahitaji ya chuo tupewe msaada wa pesa hapa na sio wanafunzi wanaoenda kupambana mtaani

Naona kwa wenzetu wanaalika watu waliofakiwa pia na kulenga wanaomaliza na wanaondoka na ujumbe gani kwa mtu aliyefanikiwa.sisi miaka nenda rudi hakuna cha maana wale wale tu.

Nini tatizo wanaalikwa watu wa waserikalini na wanasiasa, na kwanini wanaalika wageni rasmi kwa ajiri ya mgeni rasmi asaidie shida zilizopo na sio kuwasaidia hasa wale watu wanoenda mtaani,

mliowahi kusaidiwa vipi? Shida zenu zimeisha?

Huo ndio utaratibu au ni mimi tu ndio sijui au ni mitazamo tu ya watu wanafanya wanavyojisikia?.

Sijakataa kualikwa kwa baadhi ya wana siasa/wakuu wa wilaya/wakuu wa mikoa lakini wawe watu waliofakiwa kwenye jamii yetu kwamba huyo mtu alishawahi kufanya jambo Fulani na sio tu unaalikwa aongee na watu na wakati bado na yeye unajitafuta.

Ni hayo tu wakuu.
 
Tutawaalika Kibajaji na msukuma darasa la saba waliofanikiwa kutobowa kimagumashi na sasa ni wabunge.
 
Watu wa kuwaalika ni kama Mexece Melo, Yule jamaa wa Max Malipo, Millard Ayo, Mo Dewji, nk.. Kwa hao jamaa wahitimu wanaweza okoa kitu cha maana kwenye hotuba zao.

Ukimualika Mkuu wa Mkoa hakuna cha maana atachoongea zaidi ya kuwasihi vijana waitii serikali. Kiufupi anakuja kuwajaza nidhamu ya woga.
 
Tatizo hata ukiita watu tofauti nao wakifika wataanza kumwaga sifa kwa Wanasiasa + Rais na Chama tawala,

kwahyo hakuna kitakachobadilika hapo....kiufupi mambo ya ugeni rasmi kwa africa ni kama Usanii tu na kupotezeana muda bora hii kitu ifutwe tu.
 
Labda wanasiasa ndio hao hao waliofanikiwa kimaisha
 
Umewaza nje ya box.
Ilitakiwa kweli wawe wanaalikwa watu waliofanikiwa kwenye biashara fulani au projects fulani au ubunifu fulani.
Najua ni ngumu kuwapata watu kama wakina Bakhresa na Mo dewji ila angalau kuna wale wenye mafanikio ya saizi ya kati.
Nadhani tatizo kubwa kwa jamii yetu ni kukosa exposure na elimu bora yaani jamii yetu imekariri kwamba ili ufanikiwe na kuwa mtu muhimu basi ni lazima ugombee kuwa diwani,mbunge au uteuliwe kuwa mkuu wa wilaya upeo wao ndio umeishia hapo.
 
Wakuu Habari zenu?

Kuna kitu hapa kwa wageni wahalikwa kwenye mahafali ya wanafunzi wa kumaliza chuo kikuu au shule hizi za secondary. Hivi ni kwa nini wasialikwe watu waliofanikiwa kimaisha ili waongee na wanafunzi hao na badala yake mnawaalika wanasiasa na wakuu wa mikoa kuja kutoa hotuba hapo kimsingi hawana chochote cha maana chakujifunza kutoka kwao?

Inamaana hakuna watu waliofanikiwa kwenye nchi yetu wanaweza kuongea na wanafunzi wetu? Sasa sijajua wanawaalika hao wanasiasa sana ili sijui wakielezea na shida zao waweze kusaidiwa lakini mbona muda mwingine hawatoi chochote wanatuachia maneno ambayo hata yeye mwenyewe bado anajitafuta kwenye game.

Leta watu waliofanikiwa kwenye lolote lile halafu kupitia kufanikiwa kwake anatufundisha kuzingani vitu gani na sisi tunaotoka chuo/mashuleni tuzingatie hiyo vitu japo kwa uchache tu.hapo inakuwa rahisi kukumbuka .

Nasio kusikia historia ya Maisha ya mtu aliyefanikiwa kwenye mahojiano ya vipindi vya television tu na kusema nchi hii watu historia zao hawaweki wazi, wakaweke wazi wapi sasa?

Mfano Samatta au millardayo(unaweza kuchagua na wewe wa kwako wengine ), hata nawafanya biashara, watu wengine kwenye kila sehemu walishakuwaga the best au sasa hivi ni bora wahalikwe waje waelezee wakonnect mafanikio yao na ushauri wao kwako wewe wanafunzi unaenda kupambana uraiani atleast tungepata kitu na tungekuwa tunatunza kumbukumbu na sio hao wanasiasa na wakuu wa mikoa ndio watoa risara na baada ya hapo hakuna cha maana anasubiria kuteuliwa tu.

Naishiaga tu kuwaonaga kwenye list ya influencer 100 Tanzania Fulani yupo bhana, sasa hao watu wengi wao wanakuwa wamefanikiwa kwenye kitu Fulani yapo sio kivile, ila ndio watu tulionao kwa sasa, na sio kualika watu wa hovyo hawana msaada wowote kwa wanafunzi, bali chuo/shule.

Shule /chuo inaalika mgeni rasmi kwa wahitaji ya chuo tupewe msaada wa pesa hapa na sio wanafunzi wanaoenda kupambana mtaani

Naona kwa wenzetu wanaalika watu waliofakiwa pia na kulenga wanaomaliza na wanaondoka na ujumbe gani kwa mtu aliyefanikiwa.sisi miaka nenda rudi hakuna cha maana wale wale tu.

Nini tatizo wanaalikwa watu wa waserikalini na wanasiasa, na kwanini wanaalika wageni rasmi kwa ajiri ya mgeni rasmi asaidie shida zilizopo na sio kuwasaidia hasa wale watu wanoenda mtaani,

mliowahi kusaidiwa vipi? Shida zenu zimeisha?

Huo ndio utaratibu au ni mimi tu ndio sijui au ni mitazamo tu ya watu wanafanya wanavyojisikia?.

Sijakataa kualikwa kwa baadhi ya wana siasa/wakuu wa wilaya/wakuu wa mikoa lakini wawe watu waliofakiwa kwenye jamii yetu kwamba huyo mtu alishawahi kufanya jambo Fulani na sio tu unaalikwa aongee na watu na wakati bado na yeye unajitafuta.

Ni hayo tu wakuu.
Shilole, doto magari, baba levo na mwijaku
 
Back
Top Bottom