Tunachemsha kwenye utalii kwasababu:
1. Miundo mbinu mibovu, hotel chache na zingine ama mbovu au zina huduma mbaya,
2. Kujitangaza si sana, vivutio vinavyotangazwa sana sana mlima kilimanjaro,
zanzibar, ngorongoro, manyara na serengeti. Promotion ya vivutio vingine,
hakuna.
3.Vivutio vya sehemu nyingine, ndio kama hivyo, havifikiki, mtalii gani ataenda
Gombe kuangalia sokwe kama sio jangili?
4.Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye sekta hii ya utalii, wanategemea tu mtu
aje apande mlima kilimanjaro halafu arudi zake kenya kabla ya kwenda ulaya. We
are hopeless.
Tumeshindwa kuendeleza natural sceneries zikavutia. Wangekuwa ni wazungu
wangeteneza sehemu kama matema beach, mbamba bay na itungi port (Ziwa
Nyasa) na kuwa sehemu za kutalii na kutanua; visiwa vya ukerewe, ukala, na
visiwa vingine ndani ya lake victoria, visiwa vya mafia, vyote pamoja na miji ya
pwani ingetengenezwa vizuri-weka hoteli safi, beach bomba, watalii wajimwage.
Ni lazima serikali iwekeze kwa nguvu kwenye miundombinu pamoja na matangazo.
Sorry nimeandika haraka haraka.