Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Kilimo Cha Bangi kinatumika nchi Mbalimbali na jinsi siku zinavyokwenda ndivyo Mataifa mengi zaidi yanaruhusu kulima n kuvuta Bangi. Tanzania sisi msimamo wetu ni kuwafunga wavutaji na wauzaji miaka 30, kuchoma moto mashamba nakutumia mabiliaoni kupambana na raia wanaolima wakauze kwenye soko la Dunia.
Naomba anayejua Kwanini sisi tunadhani Bangi siyo zao la biashara? Je, kesho Dunia ikipitisha Bangi kuwa zao la biashara tutaendelea na msimamo wetu? Ni yapi madhara ya watu wetu kulima Bangi?
Mapombe makali tunaruhusu watu wetu wanywe, sigara hata zisizo na vichingi tunaruhusu ziingie nchini kisa wamezalisha wazungu, lakini gongo na pombe nyingine za kienyeji tunapiga marufuku badala yakuzitengenezea ubora na vifungashio, tumelogwa?
Hivi ni wapi wavuta Bangi wameonekana kuwa na madhara kuliko walevi wa pombe Kali za viwandani ikiwemo viroba?
Tunasubiri Bangi izalishwe Kwa wingi na kuingizwa kwenye viwanda vya madawa kutengeneza tiba ndipo tuanze kulima? Tunasubiri watupangie Bei? Uganda wanalima bangi na kuuza Ulaya na ni ndugu zetu wa karibu, je wao wamekuwa vichaa kuliko sisi? Kwanini tunaishi hapa Duniani kukomoana na kukaririshana maisha?