tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Nimekuwa nikifuatilia kwa muda mrefu kuhusu namba za simu zinazofanya utapeli mitandaoni, hasa kwa njia ya kuomba kutumiwa pesa kwenye namba nyingine. Mara nyingi, namba zinazohusika na utapeli huo ni za TTCL. Watu wengi wamekuwa wakitoa taarifa kwa kutuma namba husika kwenda 15040, ambayo ni huduma maalum ya kuripoti matukio ya fraud. Ingawa watu wamekuwa wakitoa taarifa hizi mara kwa mara, wengi wanasema hawajawahi kupokea ujumbe wowote unaosema kuwa huduma ya namba ya TTCL inayohusika kwenye utapeli imezuiwa.
Kwa upande wa mitandao kama Tigo na Airtel, mara kadhaa utaona ujumbe kwamba namba hizo zimesitishwa huduma baada ya kuripotiwa. Hata hivyo, huwezi kuwa na uhakika kama kweli zimesitishwa, lakini angalau kuna mrejesho. Lakini kwa TTCL, hali ni tofauti. Namba za TTCL zinaendelea kufanya shughuli hizo hata baada ya kuripotiwa mara kadhaa. Swali linabaki, kwanini mtandao wa TTCL hauchukui hatua za kuzifungia namba za simu ambazo mara kwa mara zimeripotiwa kuhusika na utapeli?