Kwanini tunaendelea kupakana rangi vidoleni punde baada ya kupiga kura 2020 licha ya kuenea kwa teknolojia hii ya alama za vidole (Fingerprinting)?

Kwanini tunaendelea kupakana rangi vidoleni punde baada ya kupiga kura 2020 licha ya kuenea kwa teknolojia hii ya alama za vidole (Fingerprinting)?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini bado tunaendelea kupakana wino/rangi vidoleni punde baada ya kupiga kura 2020 licha ya kuenea kwa teknolojia hii ya alama za vidole (Fingerprinting)?

(1) Nini mantiki ya kupaka rangi kidole cha mpiga kura ilhali jina moja haliwezi kujitokeza sehemu mbili?

(2) Kama suala ni kuzuia mtu kupiga kura mara mbili kwanini kwa maeneo ya mijini watu kusiwe na database ya wapiga kura pamoja na alama zao za vidole ili kwamba kupnde baada ya zoezi mtu anaweza alama za vidole vyake katika mashine maalum hivyo hata akienda kwingine kupiga kura mitambo inakataa kumruhusu kufanya hivyo?

(3) Kama haiwezekani. kwanini kusiwe na mashine kama zile za traffic kiasi kwamba mtu akimaliza kupiga kura kadi yake inachomekwa humo na kupewa ticket kisha anaondoka.

HAYA NI MAWAZO YANGU TU WAKUU, I STAND TO BE CORRECTED.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Wazo lako zuri. Hii ingesaidia mtu kupigia kura mahala popote.
 
Ukienda kupiga kura ukaambiwa mtandao mbovu hamna njoo baadae utaelewa kweli mkuu au itakuwa patashika
Unangojea tu mpaka Network irudi mbona kwenye ATMs watu wanasubiri. Kwanini mtandao uwe mbovu siku moja tu ya kura?

Kama imewezekana kwenye kumiliki train ya umeme kwanini tushindwe kuwa na scanners tuachane na kupakana wino?
 
Hilo haliwezi tekelezeka kamwe, hivi unajua utamu wa madaraka au cheo? Unajua utamu wa V8 wewe?, unajua utamu wa kusema jambo na linatekelezwa muda huo huo bila kupingwa? ndo mtu akuletee wazo eti tunataka tuondoe wini tulete fungerprint si unaweza kata huo ulimi na kutoa hayo macho kesho ashindwe toa hilo wazo tena.
 
Back
Top Bottom