Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HOFU HII INAYOPELEKEA KUFUTA HISTORIA YA KWELI NINI SABABU YAKE?
KITENDAWILI: KUNA HISTORIA YA TANU ILIYOASISIWA MISHENI YA TOSAMAGANGA NA KUNA HISTORIA YA TANU ILIYOASISIWA NA ABBAS MAX IRINGA MJINI UPI UKWELI?
www.jamiiforums.com
Mzungumzaji hapo juu akiwa ndani ya kanisa anaeleza historia ya TANU iliyoasisiwa Misheni ya Tosamaganga, Iringa.
Hapo chini nimeweka historia ya TANU Iringa iliyoasisiwa na Abbas Max:
https://m.facebook.com/story.php?
story_fbid=pfbid02rZviptA2cSKUJqWuZ9nwRtCfvQUi5KoYxkKEUjzVQ7UMbYJLF22BYfXtDd1ophAul&id=100022121633704
Historia ya TANU Iringa inaanza na kurudishwa kwa fuvu la Mtwa Mkwawa Iringa mwaka wa 1955.
Chief Adam Sapi Mkwawa aliwaalika Abdul Sykes na Dossa Aziz Kalenga katika sherehe hiyo ya kupokea fuvu.
Abdul Sykes na Dossa Aziz ni katika waasisi 17 wa TANU Dar es Salaam mwaka wa 1954.
Wakiwa faragha na mwenyeji wao hawa wageni wawili wa Chief Adam Sapi wakamfahamisha mwenyeji wa kuhusu TANU waliyoasisi Juius Nyerere akiwa rais wake na madhumuni ya chama kile.
Mwaka uliofatia wa 1955 Abdul Sykes alikuwa anakwenda Njombe akafikia nyumbani kwa Abbas Max na kulala hapo.
Abbas Max akaamua siku ya pili kumpeleka rafiki yake Njombe na gari yake Peugeot 203.
Walipokuwa njiani wanakwenda Njombe ndipo Abdul Sykes akamweleza Abbas Max kuhusu chama cha TANU na madhumuni yake.
Abbas Max akamwambia Abdul Sykes amwambie Julius Nyerere aje Iringa kwani yeye ameamua kujiunga na TANU na kusajili tawi la TANU hapo mjini.
Julius Nyerere alifika Iringa na akapokewa na Abbas Max.
Hivi ndivyo TANU ilivyoasisiwa Iringa na kuenezwa Jimbo la Nyanda za Juu.
Hiyo TANU iliyoasisi na Nyerere Tosamaganga Mwalimu aliasisi na watu gani?
Kulia ni Abbas Max na Julius Nyerere
KITENDAWILI: KUNA HISTORIA YA TANU ILIYOASISIWA MISHENI YA TOSAMAGANGA NA KUNA HISTORIA YA TANU ILIYOASISIWA NA ABBAS MAX IRINGA MJINI UPI UKWELI?
Historia Mpya ya TANU na Uhuru wa Tanganyika