Kwanini tunamuonea Joti?

sangujoseph

Senior Member
Joined
Nov 30, 2015
Posts
164
Reaction score
183
By Sangu Joseph

Siku kadhaa Nyuma nilipata muda wa kutafakari kwa kina kuhusiana na Mchekeshaji Joti, nadhani kama Heshima anayopewa siyo anayostahili hapa kwetu Tanzania.

Mimi kwangu binafsi @jotiofficial ni Moja ya watu ambao wanaifanya game ya Comedy itazamwe sana Bongo, na sababu kubwa ni ubunifu wake, Joti ndiye Msanii pekee wa Comedy ambaye anaweza kucheza character zaidi ya 3 tofauti na zote ukamuinjoy yeye na kipaji chake

Joti inawezekana anaonekana wa kawaidai Sana labda Kwa sababu yeye ni mtu wa kazi na vitendo tofauti na Comedians wengine, Kwa sababu nilitafuta mahojiano ya Joti kwenye YouTube sijaona hata moja zaidi akihojiwa na Mwandishi wake #MwandishiNaNishai (Kama Una mahojiano ya Joti nitumie kuna zawadi)

Sijui nini tatizo la yeye kutokua na mahojiano yeyote je sijui hapendi, anaona anagawa Content kwengine, au wanaohoji hawajaona umuhimu wa kumuhoji Joti, walau atoe inspiration yake Kwa Vijana.

Hawa wakina @Dullvani na @JayMondy_ ukija kiundani unagundua ni Wakina Joti wanaongea Sana.

Inawezekana tukawa tunajisahau kuhusu Joti, Ila ngoja niwakumbushe huyu Jamaa alianzisha Style ya kusbtua #JotiStyle kila mtoto na watu wazima waliifanya nakumbuka mpaka kuna Ngoma moja ya CPwaa aliimba kuhusu style ya Joti, Joti huyu alizungumza kizenji kila mtu akawa anajiita Hammy J, alikuja na style ya kuweka Mwanya kwenye jino bado watu walimuiga, Joti huyu huyu ni miongoni Comedian waliopata Endosment nyingi sio Endosment za Nguo zile za Kibabe za kifadha (GSM, Tigo, Assas, DSTV, NK)

Tusimuonee wala Tusijiisahaulishe niwakumbushe Joti huyuhuyu sasa anawaibua wakina Kipnde na wenzake.

Joti anastahili heshima isije ikatokea amekwenda ndiyo tuseme Pengo lake halitazibika.


#KijanaMzalendo #IloveTZ #NaniMwanaume
 
Kiukweli mimi nakukubali sana Jotii, hasa ile tamthilia yako ya MWANTUMU

Uliitendea haki sana, sema nikuulize kitu, kwanini unajipigia promo wakati unakubalika??
Yaani yupo sehemu 3 na kama humjui huwezi mtofautisha
 
Kweli Joti anakipaji na kipawa pia
 
Mi naona Joti anapewa heshima ya kutosha tu, kuhusu mahojiano labda yeye ndio hapendi
 
Kiukweli mimi nakukubali sana Jotii, hasa ile tamthilia yako ya MWANTUMU

Uliitendea haki sana, sema nikuulize kitu, kwanini unajipigia promo wakati unakubalika??
Hahaa umesahau kumuambia alipie tangazo
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dullvan ni new version ya Joti.
 
Nawauliza nyie mnaomwonea.
 
Anajua sema kiukweli hapati anachostahili. Hata subscribers wake youtube sio wengi kivile
 
Msanii namba 1 Comedy TANZANIA
 
Hivi ile style hakuitoa kwa Fresh prince of Bel air kweli[emoji23][emoji23][emoji23]mana ile TV show ilikua ya 90s na Will smith kashtua kijoti sana mule,,,Joti alianza lini yeye,ila jamaa anajua namkubali sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…