Boss la DP World
JF-Expert Member
- Dec 12, 2021
- 2,318
- 8,464
Siku moja nilibahatika kukutana na waziri fulani (jina kapuni). Nikamuuliza kwanini Wazanzibari wanachukua ardhi yetu hapa bara wakati Wabara hatuna haki ya kupata ardhi Zanzibar?
Akanipa jibu hili "Kijana Acha CHOKOCHOKO" alinikera sana, walio kuwepo watakumbuka.
Mzee mwingine wa kanda ya Ziwa aliyekuwepo tangu enzi za awamu yakwanza nayeye aliniambia nisilete chokochoko kwenye mambo ya msingi.
Ombi langu: Umiliki wa Ardhi uondolewe kwenye suala la Muungano, Wazanzibari wakija bara tuwachukulie kama wazungu wanaokuja Tanzania nasisi tukienda Zanzibar tuwe kama watalii kama ilivyo sasa.
Hivi unajisikiaje weweukija unapokelewa vyema halafu aliyekupokea akija kwako unamnyanyapaa?
Sio siri mimi nitaona faida kwenye huu muungano siku nikinunua kiwanja Unguja bila kusumbuliwa, kitambulisho cha nida iwe ni nyaraka pekee ya kuthibitisha Utanzania wangu na nipate haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
Rais wetu bahati nzuri wewe ni Mzanzibari, mimi sina chokochoko ninachotaka ni kiwanja kama vile sisi tunavyo wauzia viwanja Wazanzibari.