Kwanini tunaogopa kifo?

Kwanini tunaogopa kifo?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Jamii kubwa ya wanadamu leo inaogopa kufa licha ya ukweli mchungu uliopo ndani yetu ambao hutukumbusha kuwa ipo siku tutakufa.

Watu wengi hatuhofii sana juu ya mchakato wa kifo ila kifo chenyewe. Hofu kubwa inayotukosesha raha wakati mwingine ni ukweli kuwa tutakufa. Ndiyo ni kweli ipo siku tutakufa tukubali tukatae.

Suala hili limenifanya kufuatilia magundisho mengi sana juu ya kwa nini tunaogopa sana kufa?. Katika kufuatilia kwangu nimekutana man magundisho ambayo nimeona yanajaribu kuufunua uhalisia katika namna ya tofauti kidogo hivyo nikapata msukumo wa kuuleta uzi huu kwa wanajamvi ili kujaribu kushehenesha maarifa zaidi.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Sri M ( Master Yogi) alipoulizwa ni kwa nini watu huogopa kufa alisema “.. tunaogopa kufa kwa sababu tunafikiri sisi ni miili tuliyonayo, tunafikiri mwili ukifa na sisi tumekufa

Huyu Guru (Master Yogi) anaamini kuwa mtu hufanya zoezi la kufa kila siku kupitia usingizi mzito “deep sleep”. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa watu hawaogopi usingizi mzito kwa imani kuwa wataamka tena. Kifo ni sawa na usingizi mzito
 
Back
Top Bottom