Kwanini tunasherehekea Christmas? Sababu 10 za kiroho na kiafya

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
1. Kuzaliwa kwa Yesu ni habari njema ya furaha kuu(Luka 2:10-11).
Malaika walipoleta habari ya kuzaliwa kwa Yesu walisema hiyo ni habari ya FURAHA KUU. Na kwamba furaha hii kuu itakuwa kwa watu wote. Kusherehekea Christmas ni udhihirisho kuwa tumeipata furaha kuu katika mioyo yetu.

2. Kutimizwa kwa Unabii
Kuzaliwa kwa Yesu kunatimiza unabii wa Agano la Kale kwamba Yesu atazaliwa kwa ajili yetu(Isaya 9:6), na hiyo inadhihirisha wazi kuwa ahadi za Mungu ni kweli tupu. Kwanini basi tusisherehekee Mungu anapotutimizia kile alichotuahidi?

3. Neno kufanyika Mwili
Tunasherehekea Christmas kwa sababu Neno alifanyika mwili na kukaa kwetu(yaani Mungu pamoja nasi). Kukaa pamoja na Mungu aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, hili sio jambo dogo. Ni tukio zito linalotupa sababu ya kushangilia. "Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake,...amejaa neema na kweli"(Yn 1:14).

4. Zawadi ya Wokovu
Yesu alizaliwa ili tupate wokovu(Mt 1:21). Ilikuwa tuangamie katika moto wa milele kwa sababu ya dhambi zetu lakini Mungu akatupenda akamtoa Yesu aje kutuokoa(Yn 3:16). Kwa kuzaliwa Yesu, tumepata wokovu kwa neema. Hii ni zawadi kubwa kupita zote. Kwanini tusisherehekee?

5. Kusherehekea Christmas ni njia ya kumtangaza Yesu ulimwenguni(Mt 28:19).
Kuna watu wanasherehekea sikukuu hii bila kujua ina maana gani. Sisi tunaojua, tusherehekee na kuwaambia watu hao maana halisi ya Christmas. Tuwaambie wampokee Yesu kwa imani ndani ya mioyo yao, wapate wokovu.

6. Yesu ni Mfalme wa Wafalme.
Christmas ni sherehe ya kuja kwa Yesu, Mfalme wa Wafalme. Wafalme wa dunia hii wakienda mahali wanapokelewa kwa shamrashamra nyingi na vifijo. Kwanini sisi tusishangilie kuja kwa Mfalme aliye juu ya Wafalme wote? "Furahi sana, Ee binti Sayuni; piga kelele Ee binti Yerusalemu; Tazama, Mfalme wako anakuja kwako, ni mwenye haki, naye ana wokovu..."(Zekaria 9:9)

7. Umoja na upendo kwa Waaminio
Yesu alituombea tuwe na umoja na pia tupendane. Christmas ni sikukuu inayowakutanisha watu katika maeneo mbalimbali duniani, wanakula na kusherehekea pamoja kwa upendo na umoja. Mwimbaji wa Zaburi aliimba: "Tazama jinsi ilivyo vema ndugu wakikaa pamoja kwa umoja..."

8. Christmas ni ushindi dhidi ya giza(Yn 1:5).
Kuzaliwa kwa Yesu kumetuletea nuru. Tuliokuwa gizani sasa tunaishi katika nuru.

Nimekutajia sababu za kiroho. Sasa nakutajia sababu mbili za kiafya zinazotufanya tuone umuhimu wa kusherehekea Christmas.

9. Sherehe inaongeza afya ya akili.
Ukisherehekea sikukuu hii pamoja na wenzako, utajikuta unacheka na kufurahi. Mambo hayo yanapunguza kiwango cha msongo wa mawazo. Kisayansi, ukifurahi na kucheka unapunguza homoni inayoleta msongo wa mawazo(stress). Badala yake, furaha na kicheko vinaongeza viwango vya "endorphins, dopamine na serotonin" katika akili. Matokeo yake utakuwa na hisia nzuri na kupunguza uwezekano wa kupata hatari ya mfadhaiko wa akili(depression) au huzuni ya muda mrefu inayowafanya watu kudiriki hata kujiua, wakidhani kwa kujiua watapumzika! Anayejiua anajipeleka mwenyewe jehanum kwenye mateso ya milele.

10. Sherehe inaimarisha mfumo wa kinga mwilini.
Sherehe inayohusisha vitendo kama vile kucheza na kurukaruka kwa furaha inaweza kuongeza uimara wa kinga dhidi ya magonjwa. Utafiti umeonyesha kwamba mtu akiwa na hisia chanya inayotokana na sherehe anafanya mwili wake uongeze uzalishwaji wa seli za kinga zinazoua vijidudu vinavyoshambulia mwili na hivyo kuufanya mwili uepuke magonjwa.

Hizo ni baadhi tu ya sababu zinazotufanya tusherehekee Christmas. Kwa sababu hizo naamini umeona sasa umuhimu wa kujumuika na Wakristo wote ulimwenguni kusherehekea sikukuu ya Christmas. Sikukuu hii huwa inaanzia kwanza Kanisani, kwa kumwabudu, kumsifu na kumshukuru Mungu aliyemleta Yesu akazaliwa kwa ajili yetu ili kwa kumwamini tupate uzima wa milele.

Baada ya ibada ndipo watu wanapojimwaga nyumbani, hotelini, migahawani ili kula na kunywa. Bado hujachelewa! Kama pesa inaruhusu, na kama hupati tatizo ukila nyama, nunua nyamachoma, ule na kufurahi na wenzako. Ila tafadhali(please, please), kwa heshima zote nakusihi usisherehekee kwa kufanya tendo lolote linalomchukiza Mungu kama haya yaliyoandikwa katika Gal 5:19-21:

"Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu."

Mungu akulinde, Mungu akutunze, akuwezeshe kusherehekea Christmas hii kwa amani na furaha kuu, na akujalie kuumaliza salama mwaka huu. Merry Christmas & Happy New Year!
 
Natafutie popote kwenye biblia pameandikwa Christmas
Au hata tarehe 25 December

Upo kwenye matrix na umejaa kweli
 
Huna point .
Andika sababu zinazo prove kwamba yesu christo alizaliwa December 25 .
Umeandika makorokocho.
 
Mambo za imani bana inahitaji imani kubwa sana kuamini kuwa Mungu nae alizaliwa na hivyo ana birthday
 
Mungu kamuumba mwanadamu na akazaliwa na mwanadamu hii kitu inahitaji D kama kumi hivi kuielewa
 
Natafutie popote kwenye biblia pameandikwa Christmas
Au hata tarehe 25 December

Upo kwenye matrix na umejaa kweli
Nitafutie popote kwenye Biblia palipoandikwa Jamiiforums
 
Back
Top Bottom