Kwa sababu matokeo ndiyo kiashiria cha kushuka kwa elimu, full stop!
Dume, hebu rudia tena. Inawezekana, kuna kipimo bora zaidi cha elimu zaidi ya mtihani. Kumbuka, unakaa darasani kwa mamia ya masaa kwa miaka minne, ama saba, kwa mwanafunzi wa shule ya msingi, kisha unafanya mtihani kwa masaa machache tu.
Pia, tazama muda unaokuwa shule, si wote unakua darasani, kuna vitu unajifunza nje ya darasa. Nafikiri elimu ni kujifunza, hii ni tofauti na kujiandaa kwa ajili ya mtihani wa kuvuka darasa.
Hebu, chuja tena, tafuta mtihani uliofaulu hadi kufika hatua ya madarasa uliyonayo, kisha tazama yale uliyojifunza darasani, ulinganishe na yale unayotumia unapohitaji kufanya jambo ambalo waona ni muhimu kwa mafanikio yako--kama kufanya kwa umahiri kila kipengele cha kazi uliyoajiriwa, kuongeza kipato kwa kufungua project, mahusiano na watu, networking, afya ya familia yako, pengine hata starehe. Unafikiri bila huo kupasi huo mtihani, ungekuwaje? Ungeshindwa vile unavifanya sasa hivi?
Au, je kwa kupasi mtihani umevifanya kwa umahiri zaidi? Ukimaliza kufikiri hilo, hebu ona wale uliowaacha nyuma kimadarasa, je wameshindwa kupata mafanikio? Je, kila mahali ulipoenda ili kutafuta fursa za maendeleo mtihani uliofaulu ulikusaidiaje? Ama ni jumla ya mafunzo yako, tangu nyumbani, mazingira ya shule, na wepesi wa kutia katika maisha kile ulichojifunza ndio uliokutoa kwenye hatua moja hadi nyingine ya mafanikio yako.