Historia inaonyesha tuliwafukuza wazungu baada ya uhuru Tanzania. Serikali ya ujamaa ilivichukua viwanda vyote vya wazungu ili iviendeshe. Haya yalikuwa mawazo ya Marxism written theory, kwamba wazungu (north) wanaziibia nchi maskini (south). Baada ya muda mrefu Ujamaa ukatushinda. Mwinyi alipokuwa rais akaanza na sera za free market capitalism. Sasa kwanini serikali haianzishi viwanda halafu baadaye wakavibinafsisha kwa Watanzania? sasa hivi tunawaita wazungu warudi bongo waje kuekeza. Wazungu kuja kuekeza TZ, ni sawa na kuwaita wakoloni warudi tena kuja kutunyanyasa bongo.
Hii ni mada nzuri na nzito.Mkuu Shamu ni vyema umeileta ingawaje blogu hii haitoshi kuichambua mada yenyewe.
Mkuu Shamu amegusia siasa na kuichanganya na uchumi, si vibaya maana siasa ndio uchumi wenyewe.
Socialist economy ya wakati wa mwalimu, baada ya uhuru, ilitilia maanani ya kuwaendeleza watu sana sana katika elimu na kuondoa magonjwa.Mikakati ya kuondoa umaskini ilikuwa katika kugawana kidogo kilichopo na sio kutilia mkazo uzalishaji wa mali kibinafsi.
Mikakati ya elimu haikuwa mibaya, mtu wa Kagera alisoma Rungwe na mtu wa Tandahimba aksoma Arusha.
Lazima tukubali kuwa umoja wa kitaifa ulipatikana katika mkakati huo, ikiwa ni pamoja na kuondoa ukanda ,udini, ukabila n.k.
Kasheshe ilikuja katika uchumi.
Watu walikazania kugawana umaskini.Viwanda vichache vilivyotaifishwa vilijaza wafanyakazi kupita hata uwezo wa kuwalipa mishahara.Hata vile vilivuyoanzishwa na serikali vilijaza watu kupita kiasi.
Tatizo likawa viwanda na mashirika hayo yakakosa tija kabisa.Na katika hili hakuna shirika/kiwanda kilichopona, wafanyakazi wakaanza kuviibia na kujichotea kama ni mali zao.Hapakuwepo na uchungu pale maana mali ilikuwa haina mtu.
Mzee Ruksa akabadili mwelekeo wa uchumi kwa kuingiza ushindani, mwenyewe alisema anafungua madirisha ili hewa nzuri ipate kuingia!
Ushindani wa wafanyabiashatra ukaanza kuua taratibu mashirika yanayo endeshwa kizembe.
Hata yale yaliyokuwa yakiheshimika(NBC,BIMA,BORA etc) yaanza kudorora.
Wakati huo huo wananchi walio wengi wa Tanzania bado walikuwa wakiendelea kulala kwa kutojiingiza kikamilifu katika uchumi.
Mzee Mkapa kaingia, yeye akayauza kabisa mashirika yote.
Mimi nafikiri hapa ndio kosa letu lilipoanzia.
Mawazo ya wanasiasa wengi ni kuwa ili tuendelee twahitaji wazungu,Ni kosa kubwa , tunachohitaji ni mtaji, namna ya kuupata ndio ujanja.
Kuna viwanda /mashirika mengi yaliyouzwa ambayo sasa yamekuwa magodown/ghala za kuhifadhi mali za wajanja waliyoyanunua mashirika hayo.
Si kweli kuwa wazungu ndio wataiendeleza Tanzania bali waTanzania wenyewe.Inabidi waTanzania wajiwezeshe kupata mitaji ambayo itatumika ipasavyo kwa maendeleo.Kwa maoni yangu ni aibu kwa Mtanzania aliyejiwezesha kupatamtaji(hata huo usio halali kama EPA) kukata kiu ya umbumbu wa anasa kwa kuagiza magari ya kifahari kama Vogue au Mercedes Benz S Class badala ya kureinvest.
Hata kabla ya uchumi wa dunia kuzorota bado waTanzania tungeweza kupata mitaji kutoka kokote duniani kwa collateral ya mali iliyopo nchini.
Vilevile kuna kila sdalili kuwa waTanzania nao wana kiu ya kuwekeza.
Ule uuzaji wa hisa katika makampuni makubwa kama TWIGA CEMENT na hata megine umeweza kuonyesha kwamba kuna idle capital nchini inayoweza kutumika vizuri, ni uhamasishaji na uhakikisho kuwa fedha ya mwekezaji , hata ikiwa ndigo itarudi na faida.
Na hili ndio somo kubwa tunalolikosa waTanzania.