Samahani mkuu, hii nayo ni siasa?..[/QUOTE]
Hippo; Siasa ni imani na imani inatokana na kuamini yale yatarajiwayo ambayo tunayapata katika vitabu vitakatifu. Waumini wa IMANI ya DINI ndio waumini wa SIASA. Karibu twende kwenye uchaguzi.
Mkuu Miwatamu, niliuliza kwani swali limekaa kama hoja!
Anyway nadhani kuna jambo fulani( Ujinga-kutokuwa na ufahamu au uelewa wa jambo fulani).
Kwa kawaida katika Kuomboleza(Mourning) kuna kupitia hatua tano..
Denial, Anger, Bargaining, Depression, Acceptance.
1.Denial(Kutokubali)
Ambayo huwa kama temporary defense kuwa, hii haiwezi kutokea(Wakati mwingine hata kama watu walitarajia kifo hicho)
2. Anger(Hasira):
Hasira huja hasa, mtu/watu wakijiuliza kwanini mimi/sisi?,
kwamba hakuna usawa katiak hili(it's not fair)..mtu/watu huwa na hasira dhidi ya wengine au wao wenyewe!
3. Bargaining(Kuomba):
Mtu huwa radhi kufanya chochote, ..mawazo na mtazamo wa nitauza hata nyumba yangu/gari/ nitatumia akiba yangu yote kufanya/kuepuka kutotokea kwa kifo!
4.Depression
🙁Kudhoofu kwa kusononeka)
Mtu huepuka wale wanaokuja kumuona kwa kusudi la kumfariji(kuhani), marafiki na jamaa..mara nyingi huwana mawazo hasi kuhusu msiba, "kwa nini kuhangaika kote anyway?" ,"Haitasaidia lolote", "Ni kazi bure" n.k
Acceptance:
Mtu hukubali kuwa yaliyotokea yametokea, na hana uwezo wa kuyabadilisha ila kuendelea na maisha na kujifunza kutokana na msiba(kifo) hicho!
So, naamini baada ya muda "wanandugu hao wataelewa"..POLE kwao kwa msiba.