Kwanini tusiamini kuwa kufa kupo?

Miwatamu

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2012
Posts
1,450
Reaction score
489
Nimeamua kuamka na swali hili baada ya ile habari ya wana ndugu wa marehemu aliyefariki tangu Ijumaa ya wiki hii kukataa kuamini kuwa amekufa na kuamua kumpeleka katika Kanisa la Ufufuo na Maombezi ili arudi kuwa hai. Je, pamoja na sisi kushinda na kukesha makanisani na misikitini bado tu hatuamini kuwa kuna kuzaliwa na kufa?
 
Samahani mkuu, hii nayo ni siasa?..[/QUOTE]

Hippo; Siasa ni imani na imani inatokana na kuamini yale yatarajiwayo ambayo tunayapata katika vitabu vitakatifu. Waumini wa IMANI ya DINI ndio waumini wa SIASA. Karibu twende kwenye uchaguzi.
 
Kama kufa ni lazma, basi na kuokoka ni lazma
quoted
 
Hao wanapingana na agizo la Bwana wa Majeshi. Angalikuwa hai wangalifunga na kuomba Mungu angalikubali angaliahirisha kwa muda tu lakini kufa ni hakika.
 
Kwanza kama wanampeleka akaombewe ili awe hai, maana yake wanakubali kwamba amekwisha kufa, vinginevyo hayo maombezi ni usumbufu kwa wachungaji, waombolezaji na Mungu mwenyewe. Haya basi, kufa si swala la kuamini ni swala la ufahamu. Tanaamini yale ambayo hatuna uhakika wa kisayansi nayo, lakini kufa tunaweza kuhakikisha. Kwa nini tujisumbue kuamini? Ngoja ufe, halafu uendelee kuwa na mashaka kama umekufa au bado!!
 
 

Amepekwa kwa Bwana ili amfufue.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Labda wanamdai,sasa wanahisi amevunga kufa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…