#COVID19 Kwanini tusishindanishe mawazo yetu kuhusu juu ya chanjo ya Covid-19 kwa uwazi?

#COVID19 Kwanini tusishindanishe mawazo yetu kuhusu juu ya chanjo ya Covid-19 kwa uwazi?

lendila

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
5,806
Reaction score
4,370
Kwanini kama taifa huru tusishindanishe mawazo yetu kuhusu usalama wa chanjo ya corona kama inafaa au haifai?

Kama tutaona chanjo ya corona inafaa kwa afya zetu iletwe nchini tuchanjwe.

Kama chanjo itakuwa haifai tuikatae chanjo kwa uwazi na kwa umoja wetu kama taifa moja la Kambarage.

Watanzania ni watu wapole sana.

Watanzania ni watu wakarimu sana wakipata muda wa kushindanisha mawazo yao kwa amani upendo na mshikamano tutafikia muafaka mzuri sana kuhusu chanjo ya corona.

Haya ni maoni yangu binafsi.

Mwenye maoni tofauti karibu uchangie maoni yako.
 
Leo kina masanja wanagawa barakoa kuna nini?
 
Hakuna mtu anayekataa dawa ila kwenye Corona walishakosea wenyewe kitambo waliposema wa AFRICA tutaongoza kwa kufa pale ndo walijichanganya na hawana lengo zuri kwetu.
 
Back
Top Bottom