Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Biashara zinaendeshwa Kariakoo kwa sasa hazina tofauti na biashara zilizokuwa zinafanyika miaka ya 1990 za ulanguzi.
Soko linazidi kudorora, maduka yenye hadhi yanazidi kupotea na kuzaliwa vibanda vidogo vidogo visivyo kidhi.
Mpangilio wa biashara nao unachangia soko kukosa mvuto huku bidhaa zenye ubora mdogo zikipewa kipaumbele.
Matokeo yake ni kuibuka kwa wafanyabiashara wachache waliopo serious wanaokwenda kwenye masoko nchi jirani kuchukua bidhaa na kuziingiza nchini kinyemela kisha kuziuza kwa bei kubwa kwa wateja serious.
Upotevu huu wa mapato unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kodi nyingi, kukosekana kwa viongozi imara na sera mbovu.
Nchi nzima kuna maduka ya nguo za hadhi yasiyozidi kumi na mengi yanamilikiwa na mtu au kampuni moja. Kwanini tusiwasaidie Watanzania kufungua maduka yaliyopo kwenye ulimwengu wa kwanza hapa nchini?
Mawaziri na viongozi wengine wanaolipwa vizuri wanaenda kununua nguo nje. Kwanini badala ya kununua nje, wasitengeneze mazingira ya biashara kama ya nje? Tulitegemea kwa kuwa na bandari, watu wa madaraja yote wangeingia nchini kufanya biashara, ila sivyo. Tumebaki kutukuza vya Uturuki, Dubai na kadhalika.
Tubadili fikra.