Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Uamuzi wa Zitto kuleta hoja ya kutaka iundwe Kamati Teule kuchunguza mambo yanayohusiana na utoroshaji wa fedha na ufichwaji wa fedha hizo kwenye akaunti za nje ya nchi unahitaji kupongezwa. Zitto ameweza kutuonesha baada ya kutudokeza kwa muda kuwa tatizo ambalo tumekuwa tukilizungumzia kwa muda la ufisadi limejikita mno katika watawala wetu na sasa limeota mbawa hadi ngambo.
Zitto ameweza kutuonesha kwa kutudokeza akitumia taarifa mbalimbali ambazo kwa kutumia uzoefu wake ameweza kuzipata kuwa kuna mabilioni ya fedha za Watanzania yamekwapuliwa kimtindo na kufichwa nje ya nchi na baadhi ya wahusika wa mambo hayo ni watu waliowahi kushika nafasi kubwa katika utumishi wa umma. Hivyo, kuamua kuchunguza mambo haya ni jambo jema na lenye kutaka uthubutu wa kutosha.
Tusitumie Bunge kushughulikia uhalifu
Pamoja na hayo naamini kutumia Bunge kuchunguza uhalifu au tuhuma za uhalifu ni kutumia Bunge vibaya lakini vile vile ni kudhoofisha taasisi zetu au vyombo vyetu vya kushughulika na uhalifu. Ninaamini katika suala hili la Kashfa ya Fedha Haramu tunapaswa kulazimisha vyombo vyetu vya kusimamia sheria (law enforcement agencies) kufanya kazi yake na kuliacha Bunge lifanye kazi yake ya msingi utungaji wa sheria na kusimamia serikali.
Ninaamini lengo la Zitto na la wengine wenye kuunga mkono hoja hii ni kutaka uhalifu huu uchunguzwe na wahalifu wachukuliwe hatua za kisheria. Lakini hili haliwezi na halipaswi kufanywa kwa kuepuka vyombo vya dola vyenye kusimamia sheria. Ni muhimu kutenganisha suala la kisiasa na lile la kihalifu.
Kwenye kesi za EPA nilipinga Rais Kikwete kuunda tume ya kuchunguza uhalifu badala ya kuviacha vyombo vya sheria kushughulikia. Ni sababu hii hii inayonifanya niamini kuwa kutumia Bunge kushughulikia suala linalohusiana na uhalifu ni kudhoofisha vyombo vyetu. Wabunge wanatakiwa kuvipa nguvu vyombo hivi na wahusika.
DPP hatumika vizuri kutumia madaraka yake
Mojawapo ya matatizo yangu binafsi ni kuwa hatujamtumia vizuri sana DPP (Ofisi ya DPP) kushughulika na uhalifu kama ambavyo sheria ilivyotoa nafasi. Katiba ya Jamhuri na Sheria ya Ofisi ya National Prosecution Service zimeweka nafasi nzuri ya wahusika hawa kufanya kazi yao inavyopaswa na wakati umefika Bunge lianze kuwakalia juu.
Sheria ya NPS inasema kuwa DPP ana uwezo wa kuagiza Polisi au chombo kingine cha uchunguzi kufanya uchunguzi unaohusiana na uhalifu (Kifungu 9, kifungu kidogo cha 1e). Kifungu kidogo cha 4 kifungu hicho hicho cha 9 kinaelekeza Polisi na yeyote anayefanya kazi za uchunguzi
Kifungu cha 16 kiko wazi zaidi kwani kinaeleza kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ana uwezo wa kumwagiza yeyote kufanya uchunguzi wa tuhuma za uhalifu ambazo zimemfikia DPP. Kwanini hatutumii kifungu hiki kumtaka Feleshi afanye kazi yake? Kwanini wabunge wasimwandikie DPP au kumwagiza rasmi kuchunguza mambo haya ya kihalifu.
Kamati Teule inafunua mengi lakini mwisho ni DPP
Sasa ninaelewa kuwa kwa kkutumia Kamati Teule tutaweza kujua mengi hadharani kwani ikimaliza kazi yake itatakiwa iripoti mbele ya Bunge na Watanzania watapata nafasi ya kujua kilichotokea na hata labda majina ya wahusika kwani wabunge wanalindwa na kinga ya Kibunge. Kamati Teule ina uwezo mkubwa wa kuchimba chini na kujua mengi kama tulivyoona kwenye kamati teule ya Mwakyembe.
Lakini mengi yanaweza kufunuliwa zaidi kwenye mahakama na siyo tu kufunuliwa lakini ushahidi mzito zaidi unaweza kuwekwa mahakamani; watu wataishwa kutoa mashahidi na watuhumiwa watapewa nafasi ya kujitetea. Msemo huu wa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni umekuwa maarufu sana na nimewahi kusema hivi majuzi kuwa haki ni haki hata ya adui yako.
Tujisjaribu kukwepa utawala wa sheria kwa kuhofia ati wataachiwa kama alivyosema Nchimbi kwenye kesi ya Mwangosi. Lengo la mahakama ni kupima ushahidi na kuutafuta ukweli. Kama DPP na wenzake hawatoleta ushahidi mzuri na watu wakaachiwa ni kosa la huo mfumo lakini kwenda tu kuchunguza na Kamati TEule halatu watu wanajiuzulu tu na kuendelea kula vya kuiba siyo haki; siyo haki kwa Tanzania na siyo haki kwa mfumo wetu wa sheria.
Bunge lifanye kazi yake lisifanye kazi ya wengine
Jambo moja ambalo Zitto amelisema nalo ni zuri ni kutaka mswada wa sheria uletwe mara moja kuweza kushughulikia mapungufu ya sheria yaliyopo sasa na hasa kuziba mianya ya sheria inayosababisha watu kuweza kutorosha fedha lakin ipia sheria ambayo itaimarisha vyombo vyetu vya uchunguzi ili viweze kuwa na triggers badala ya mtindo wa discretion ambao umewekwa kwenye sheria hizi. BInafsi naamini wabunge wanaotaka mabadiliko ya sheria hii hawana sababu ya kusubiri serikali ilete mswada wa sheria; wao wenyewe kwa kutumia madaraka yao walete mswadwa wa mabadiliko wanayoyataka na waujengee hoja upitishwe na Bunge na ukikataliwa (kama ni mzuri) kwa sababu ya kichama wananchi watajua ni chama gani kimekataa mabadiliko na kwa vile tayari inaonekana kuna uwezekano wa bi-partisan support basi mswada huo utapita tu bila kusubiri serikali.
Kwa hivi sasa hata hivyo:
a. Bunge lisiunde Kamati Teule kuchunguza uhalifu bali litoe hoja ya kumtaka DPP kuanzisha uchunguzi mara moja wa fedha haramu na kuleta mashtaka dhidi ya wahusika wote kwa kutumia uwezekano wote wa sheria (full extent of the law) na limpatie msaada wote unaotakiwa
b. Kamati Teule iundwe kwa ajili tu ya kufanya uchunguzi wa mianya ya sheria ambayo inachangia watu kutorosha fedha na kamati hiyo ije na mapendekezo na mswada wa kusahihisha makosa hayo.
c. Kama DPP hataki kufanya kazi kwa hoja ya Bunge basi Bunge liangalie namna ya kuifanyia marekebisho sheria ya NPS ili kutengeneza triggers ambazo zitamlazimisha DPP na AG kusimamia sheria kweli na siyo kufanya kazi kwa discretion yao. Haiwezekani Bunge lianze kufanya kazi ya mpelelezi na prosecutor vinginevyo tutakuwa tunalipa nguvu nyingi sana na baadaye litaanza kuunda Kamati Teule kuchunguza wizi wa mbuzi na kuku kwa sababu tu waliopewa madaraka hayo hawataki au hawaoni wanalazimika kufanya uchunguzi.
d. Kama nilivyowahi kuandika huko nyuma msisitizo mkubwa wa kibajeti na miundo mbinu umewekwa kwa polisi, TAKUKURU lakini siyo DPP. Bunge limpatie DPP uwezo wa kiutendaji na kumtengenea bajeti itakayomwezesha kupambana na ufisadi kwa kutumia mbinu za kisasa. Katika vita dhidi ya ufisadi DPP ndiye mtu muhimu zaidi siyo Hosea wala Mwema. Kwanini hatumpi vile anavyostahili? Tusimdai kama hatumwezeshi!
Kama DPP hataki kufanya uchunguzi baada ya kutolewa hoja na Bunge na licha ya kupewa tuhuma za uhalifu kama zilivyoanishwa katika hoja ya Bunge basi wanaharakati na wabunge wamtake bwana Feleshi kujiuzulu kwa kushindwa kazi yake.
Haiwezekanii uhalifu wa kila namna udaiwe kufanyika halafu DPP hata mara moja haanzishi uchunguzi wowote wala kumwagiza yeyote na badala yake tunasikia maagizo kutoka kwa Waziri, Rais n.k; anafanya nini kwenye ofisi hiyo?