Wadau wa historia ya Tanganyika mnisaidie.
Mwaka 1958 uchaguzi ulifanyika Tanganyika na TANU kupata viti 29 kati ya 30 huku kiti kimoja cha ubunge yani Legislative Council kikichukuliwa na UTP.
Mwaka 1960 uchaguzi ulifanyika tena na kipindi hiki viti vya bunge ni 71 ambapo TANU ilinyakua viti 70.
Sasa swali ni hili: kwanini uchaguzi ulifanyika tena ndani ya muda mfupi?
Baaada ya kupata tuu uhuru mwaka 1961 Tanganyika ilikua na vyama vikuu vinne(TANU, UTP, ANC, AMNUT) vyama hivi vilidumu hadi mwaka 1965..ikapitishwa sheria na mwl. Nyerere ya kuvifuta vyama vyote na kubakia na TANU pekee. Mwaka 1977 TANU (Bara ) ikaungana na ASP(Visiwani) na kuunda CCM. Mnamo mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi ulirudishwa tena kwa mara ya pili.