Mazoezi makubwa matatu yanayogharimu pesa nyingi za wananchi ni vita, sensa, na uchaguzi. Uchaguzi, kwa upekee wake, mara nyingi husababisha kuyumba kwa amani na utulivu wa nchi kama tunavyoshuhudia katika chaguzi mbalimbali. Baada ya mchakato huo, viongozi na vyombo vya dola hujiona wamemaliza jukumu zito.
Swali ni: Kwanini Tanzania tumejifungamanisha na mizunguko ya uchaguzi kila baada ya miaka miwili ndani ya kipindi cha miaka mitano? Kwa mfano, sasa tumemaliza uchaguzi wa Serikali za Mitaa (ambao si mchakato mdogo), na si muda mrefu tutaanza maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani. Je, tunataka kuwa Taifa la uchaguzi kila wakati? Miaka mitatu kazi kidogo, miaka miwili uchaguzi. Kwanini?
Ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kisheria na kikanuni ili chaguzi zote zifanyike kwa wakati mmoja, kama inavyofanyika Zanzibar.
Pia, chombo kimoja, kama Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kinapaswa kupewa jukumu la kusimamia mchakato wa uchaguzi kwa ufanisi na kwa mara moja.