Habari, nikiwa kama mpenda maendeleo na mtumiaji wa mara kwa mara wa airport ya mwanza, kwa kweli ni aibu sana kama jiji la mwanza kuwa na airport ya viwango vya chini na iliyochakaa ya sasa ambayo haiendani na viwango vya jiji.
Turudi kwenye ujenzi wa jengo jipya la abiria ya mwanza airport ambapo serikali ilipania baada ya kukamilika itakuwa mwanza airport.
Lakini jengo hili kwa zaidi ya miaka mitano sasa tumekua tukipigwa dana dana juu ya kukamilika kwake, ukipita airport ya mwanza pale utaona hakuna tena shughuli inayoendelea ya ujenzi ni kama kila kitu kimesimama.
Nakumbuka usimamizi wa ujenzi ulihamishwa kutoka jiji la mwanza kwenda mamlaka ya viwanja vya ndege lakini progress bado ni very poor!!!
Ukiangalia airport za mikoa mingine kama songwe , tabora na shinyanga zinaendelea vizuri ila hii ya mwanza imekua kama kichaka cha ufujaji wa pesa sasa.
Mamlaka zinazohusika zitoke zitueleze kulikoni? maana nakumbuka pia mkandarasi sijui pia alikopi designs za uwanja wa Heathrow Airport na mkuu wa mkoa kipindi kile alikosoa vikali (kama sijakosea kipindi cha mkuu wa mkoa Adam Malima)ujenzi ata vyoo vilikua sio sehemu sahihi, sasa sijui walifanya marekebisho au ikiwezekana watuambie kuwa wamefunika kombe mwana haramu apite
Mamlaka husika mtuambie kwa kweli wanachi tunataka kujua