Kwanini ukiishiwa pesa mipango huwa mingi?

chumanile

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2018
Posts
296
Reaction score
328
Natumai tuko salama,baada ya kuishinda cvd19.

Huu usemi wa "masikini akipata matako hulia bwanda". Sijui unamaanisha nini?mtanifahamisha wahenga.

Ila ninachojua mimi, mtu baada ya kuishiwa pesa mipango inakuwa mingi. Tena anajua mpaka dili la buku kumi akipata afanyie nini ili siku zisonge mbele.

Hapa napata maswali mengi ya kujiuliza.

Hivi ni kweli shibe mwana malevya na njaa mwana malegeza. Iweje ukiwa na pesa unajifanya hamnazo?

Hivi mipango hiyo unayoipanga ukiwa hauna pesa, usiipange ukiwa umezishika na kuzielekezaa huko? Au ulijiona wewe umepata pesa kwa akili yako ya darasani?

Hivi leo utoe mawazo kwa wenzako wakati wewe ndiyo ungekuwa mfano kipindi una pesa ili sisi tuige kutoka kwako?

NIKUPE ELIMU.
Kufanikiwa hakuhitaji elemu
Kufanikiwa hakuna ujuaji
Kufanikiwa si kwa unjaunja.
Kufanikiwa ni neema na baraka kutoka kwa M/Mungu.
Jifunze ukiwa na pesa kupokea mawazo mapya na kuzielekeza fyucha.
 
kuna wanaosemaga pesa zina mashetani....

ukiwa nazo mipango inapotelea wapi sijui, usipokuwa nazo unapiga bajeti nzuri...

ama kweli Mipango sio matumizi
 
Mwezi uliopita nilikuwa na laki tatu ambayonilipanga niitumie hadi mwezi utakapoisha (matumizi muhimu kama chakula bill ya maji, umeme, vocha, nauli n.k),

Ghafla nikapokea simu kutoka kwa anko ambaye unakazi Nzuri sana anamiliki asset mbali mbali, anko alikuwa anaomba nimsaidie kama 60k,
Kutokana na uchanga wa maisha nilionao nilishangaa sana, haraka nikamtumia

Hapo ndipo nilipobaini hali sio nzuri mtaani.
 
hapa mimi ndo nimekaa geto naona mambo hayapo sawa naweka mipango mingi ya baadae hapo mabeberu wakija kuanza kutalii tena.manz wangu ilikuw kila siku ananipa ushauri weka hichi fanya hivi namuona anazingua tuuu sababu ela ilikuwa ya kumwaga tuu.yaani hapa nimikaa geto najutia tuuuu.naombea nisije kusahau tena kuweka mambo safi magetoni
 
Na kwanini ukiwa na pesa unasahau mipango ulioweka???
 
Ukiwa huna pesa unakuwa na tabia njema! Kuwa nazo sasa hapo ndo utajua nani shetani kati ya yule alietupwa kutoka mbinguni au wewe mwenye hela😂
Tena unaweza kuta ni ya mkopo😅
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nacheka kama mazuri vile, yaani kama nakuona vile pole sana jamani huyo manzi usimwache kabisa
 
Ukipata pesa ndiyo hapo macho huwa na mwanga mkali hata kuchagua mpenzi wakuendana naye maana ulinaye wala haendani na pesa ulizo nazo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ufinyu wa elimu ya pesa ( mapato na matumizi ) ni mdogo hio ndo sababu.
 
Mi siamini iko kitu.mbona hata maprofesa wa wauchumi nao wakiishiwa hujuta na kusema hajatumua pesa vizuri?embu tafakari mkuu katika hilo
Ufinyu wa elimu ya pesa ( mapato na matumizi ) ni mdogo hio ndo sababu.
 
Hizo bando za ku comment huku + kifaa wezeshi unachotumia ndio pesa zenyewe hizo.
Huyo tayari ameshapata pesa na keshasahau kama aliyonavyo navyo ni pesa. Kweli ukiwa na pesa sometimes unasahau kama una pesa.
 
Ukiwa masikini unakuwa na plan nyingi mara nikipata nitanunua Airbus, Lexus V8 1😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…