Kwanini ulijiunga JamiiForums na uliijulia wapi?

Beira Boy

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2016
Posts
19,976
Reaction score
32,195
Aman iwe nanyi wakuu wa jukwaa katika bwana

Kama kichwa cha habali kinavyosomeka hapo juu

Kila binadamu hujiunga mtandao anaoupenda kwa wakati wake na sababu zake kuna wengine hujiunga mitandao fulan ili wapate mademu kwa urahis, wengine hujiunga ili watoe darasa na wengine ili wapige hela, hawa wanaopiga hela wana njia njia nyingi lakin wengi ni kutapel watu


Mimi nilijuanga humu ndan ili nipate kuchangia mambo fulan hasa ya din na siasa na wakati najiunga humu kipindi hicho mijadala ya din na siasa ilikuwa imepamba moto ile mbaya


Wapi niliijulia jamii forum niliijulia mozambiqe nikiwa nimekaa na masela sasa kuna jamaa mmoja alikuwa anajua vitu vingi sana kitendo kilichopelekea nimuulize wewe jamaa mambo haya huyatolea wapi jamaa alilinga kunambia lakin mwisho wa siku alinambia kuwa ni jamii forum hapo hapo nilianza kuitafuta jamii forum na kujiunga mazima

Nawe waweza sema kwanini ulijiunga na wapi kitu gan kilikushawishi

Nawasilisha

LONDON BABY

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka ilikuwa 2009 nikiwa kidato cha tano,tulikuwa kwenye gar na mke wa mjomba wangu ndo akapigiwa simu mme wake.Wakapiga story kwa muda baadae wakaanza kumzungumzia jamaa yetu aliyekuwa masomoni Marekani kwamba amerejea na bado hajapata kazi,hapo ndo huyo aunt wangu akasema labda huyo jamaa awe anapitia Jamii forum ili aweze kuona matangazo ya ajira. Hilo jina Jamii forum lilinikaa kichwani mpaka nilipoenda chuo nikawa na access ya internet ndo nikaanza kuitumia JF

senty from my Iphone 7 using jamii forum app
 
Nilikuwa namuona Jamaa flan anaingia Kwa computer, alikuwa anacheka pekeake tukimuuliza anajibu Kuna mtubkamfurahisha Jf.

Nikashawishika kuingia jf lakini nikawa siielewi,ila nikawa naingia mara chache mno.

Siku moja nikakutana na thread moja MMU iliohusu wapendanao wawili waliokuwa ktk mgogoro,jamaa akawa anaomba msaada wa wana jf wamsaidie kumbembelezea baby wake ili amsamehe.

Wahusika wote walikuwa online,hatimae walipatana.

Nilivutiwa sana aisee! Ndio nikawa member rasmi.
 
Me nilikua na mshikaji tunaOngelea mambo ya siasa kumhusu zito kabwe ndio akasema tena nimeona jamii forum huyu jamaa kateuliwa kua mwenyekiti kamati ya madini!!!!!!! Enzi izo zawahenga wakina jk..
 
Dah Nimeanza Kusoma Nyuzi Tangu 2010 Ila Sasa Vinokia Nlivokua Natumia Kipindi Icho Hata Nlikua Sielew KuRegister Na Nlikua Siwez. Bas Nkipata Access Ya Internet Nasearch Jamiiforums. Nkawa Nakumbuka Na Kusahau Nakumbuka Nasahau. Mpaka 2011 Nlipoamua Kufuatilia Seriously. Ila Kusema Ukweli Mwanzoni Nilidhani Watu Walio JF Ni Wakenya Au Watanzania Waliopo Nje Ya Nchi,Au Wasomi Sanaaaaaa!!!
Nlikua Nawaogopa Sana Yani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliijua tokea tumbon mwa mama angu nahisi alikua mtumiaji wa jf
 
hahahahahah so wewe unaogopa wasomi?

nauliza tu
 
Reactions: BAK
Ni kweli kabisa,watu wa JF zamani walikuwa wakichangia post zao zilikuwa za upeo wa hali juu sana. Sasa hivi wanafunzi wa sekondari wamekuwa wengi na kuleta mzaha.

senty from my Iphone 7 using jamii forum app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…