Kwanini uliondoka nyumbani kwenu kwenda kujipangia na hali ilikuwaje?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nilipanga geto lakini sikulala karibu wiki toka nilipie kodi, kipindi nimemaliza form 4 tayari nilikuwaga najua kunyoa maana likizo za nyuma nilikuwa nashinda sana kwa mjomba alikuwa kinyozi basi hata shuleni mimi nilikuwa kinyozi wa shule. nilipomaliza four nikiwa nasubiri form 5 niliweza kupata kakibanda kangu.

Siku niliyoamua sasa naaga nyumbani naenda kulala kwangu walishangaa naenda kupanga mbona hawajaona vitu ambavyo labda nilikuwa navyo pale home niki nunua labda kidogo kidogo, niliwaambia sihitaji mambo mengi cha muhimu mwenye ujuzi hafi na njaa,

Niliweza kununua godoro, shuka, pazia, ndoo mbili, ufagio, debe la unga, debe la mchele, kindoo cha dagaa na jiko...

Siku ya kwanza kuamka geto langu nilijiona mpya naamka asubuhi kama nipo peponi nipo huru ingawa upweke mwingi unajua ukikaa na familia inakua umezoea basi ukihama kuna kaugonjwa.
 
Nilikuwa na mademu kibao nakosa uhuru wa kunyadua coz mshua alikuwa anasheria zake home mwisho kuingia saa mbili usiku nje ya hapo tafuta pa kulala nikaona isiwe tabu nikaenda kupanga
Ila mshua alikuwa ana hofu na mimi coz nilienda kupanga nikiwa mdogo sana
Ila akujua kama mimi ni mafia 😂😂😂
 
kwasababu nilihama mkoa kabisa, Sasa ningelala ndani ya pipa?

Niliona kutoboa nikiwa mazingira ya karibu na nyumbani itakua ngumu kutoboa maana ilikua rahisi kurudisha mpira kwa kipa kuliko kukaza kuvumilia maumivu ili niende mbele

kwahiyo nikahama mkoa kabisa ili kurudisha mpira kwa kipa iwe kazi ngumu kuliko kuvumilia
 
Kuna mshkaji wangu alipanga nyumba nzima halafu familia yake ikawa ndogo tukakubaliana me anipangishe chumba kimoja, nikanunua godolo na shuka.

Nikaenda home nikawaambia me naenda kupanga wakabaki wanashangaa tu ndio ikawa mwanzo wa kujitegemea.

Baadae nikahama kabisa na mkoa.
 
Ila wazazi wengi wanakuwa na wasiwasi pale mtoto anapoenda kupanga. Ingawa ukifanikiwa ndio wanakuja elewa umuhimu wa mtoto wa kiume kuondoka nyumbani.
 
Back
Top Bottom