Habari wakuu, imekuwa jambo la kawaida kwa members wa JamiiForums kutumia majina fulani fulani hivi ambayo ni unique na tofauti kabisa na majina halisi ya wahusika.
Of course sababu kubwa ni ishu ya privacy na confidentiality ya members japokuwa sio wote wanatumia fake IDs.
Je, ni sababu zipi zilizokupelekea uamue kuchagua hilo jina kama your user ID: Kwanini uliamua kujiita pakashume, au bulicheka, au spanamalaya n.k n.k n.k.
Binafsi niliamua kujiita Orangutan kwasababu nawakubali sana hawa masokwe na ofkoz kwa namna fulani naona binadamu tunashabihiana kitabia na hawa ma-chimps (After all we are all homos: homosapiens, homohabilis, homoerectus n.k n.k). Well, vipi kuhusu ID YAKO?