GM7
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 492
- 24
Waheshimiwa sana wanaJF,
Nawauliza hasa wanaume, kwanini usimruhusu mke wako au mpenzi wako wa kike kuwa na simu ya mkononi wakati wewe unayo?
Katika tembeatembea nilikumkuta dada mmoja ambaye tunafahamiana, ana mtoto wake mmoja na ana mume. Katika maongezi mbalimbali nikamwambia siku hizi karibu mtu ana simu ya mkononi sasa kwa nini wewe huna simu kwa ajili ya mawasiliano wakati simu nyingine zinauzwa mpaka sh.10,000 tu? Akasema "ninue simu baba J atanielewa? Si atafikiri nawasiliana na wanaume wengine?"
Siku nyingine akaja mama mmoja kununua vocha kwangu. Katika maongezi naye akasema "mume wangu hajui kama nina simu ya mkononi, maana akijui tu nyumbani patakuwa hapatoshi. Yaani hapendi kabisa niwe na simu ya mkononi ila yeye tu awe anayo"
Swali kwa wanaume: Kwanini wanaume hawapendi wake zao kuwa na simu? Kuna tatizo gani mke wako kuwa na simu wakati wewe unayo?
Swali kwa wanawake:Kwa nini waume zenu hawawaamini mkiwa na simu? Mna matatizo gani yanayosababisha msiaminiwe kuhusu hili suala?
Karibu tuendelee kuchangia mada.