Kwanini unaipenda Jf

binjo

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2016
Posts
2,115
Reaction score
1,247
Binafsi ndo sehemu maalumu yakujua IQ za watanzania,ndo sehemu maalumu yakujua umbea wa serikalini,michezo na burudani,sehemu ya kujifunza majibu ovyo na chaya.

Ndo sehemu ya kujifunza Tanzania ni nchi ya aina
Ndio chombo changu cha habari kabla sijaenda buguruni kujumua bidhaa za gengeni lazima nifungue nini kimejili hata kama sina data.

WEWE JE?



Asante jf.
 
Kwa sababu wapo watu ambao kwa kiwango kikubwa ikitokea tukaenda kuishi sehemu wooote,basi itakuwa ni sehemu bora kuwahi kutokea Duniani.

Watu wa humu ni waelewa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamna sehemu yenye raha kama JF; Ni kijiwe kilicho na watu wa kila namna wasio na elimu mpaka maprofesa.

Hamna sehemu nyingine yakutolea povu na stress zaidi ya JF.

JF iendelee kudumu kwa kweli.
 
Mahali pangu pakulopka na wasinitambue,alafu natajilika kiakili,kiroho,na kikifikra. Idumu jf
 

  1. Ni darasa tosha hasa kwa Knowledge Seeker kama Mimi na Wachache wenzangu tunaojitambua.
  2. Ni mahala panapotusaidia kupunguza machungu ya kunyimwa Mbunye / Mikuyenge na Wapenzi wetu.
  3. Ni sehemu Kuu ya kupata Habari isiyo ya Kupepesa, Kutikisa wala Kumung'unya.
  4. Ni uwanja tosha wa kujua Saikolojia ya Watanzania kwa Kipindi hiki imelalia wapi na uipeleke wapi.
  5. Ni mahala ambapo panawakilisha hisia za Mamilioni ya Watanzania zilizo hasi au chanya.
  6. Ni sehemu sahihi kabisa ya Kujifunzia kuhimili changamoto za matusi na Kukukomaza Kiubishi na Kiakili.
  7. Ni mahala pazuri sana kwa Kuwajua MAPOPOMA na VIPANGA hata kutokana na michango yao tofauti tofauti.
 
JF ni pahala pa kila kitu: elimu nzuri tu, umbea, uchawi, urafiki, unafiki, ushoga, vichekesho, mtongozano, kuropoka (japo si sana, kuna bani), mapishi, kupata wake/waume, kufanya biashara, kwa ujumla JF ni rafiki kutegemea una mapenzi gani naye. Baada ya kuchoka na mihangaiko ya hapa na pale, wakati wa kujipumzisha pumzika na JF.
 


Heshima kwako Mkuu hasa 4'5'6
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Kweli kabisa muhenga.
 
Ni mahali pekee unapoweza kupata habari za uhakika asilimia100,

Vyanzo vingi vya habari hapa ni watu ambao kwa namna moja au nyingine ameiona habari kwa macho, hkuna udaku jf

Memba wengi wa hapa ni watu wenye uelewa mkubw wa mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…