Kwanini Unaogopa Kufa?

Kwanini Unaogopa Kufa?

Navoyne

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2010
Posts
874
Reaction score
373
Jamani wadau katika pita pita zangu nilijikuta katika mjadala mkali kuhusu kifo, Mjadala ulikua hivi:

1. Je watu wanahofia kufa kwa sababu ya uoga wa kutojua mbele kuna nini? (motoni na peponi) au

2. Watu wanaogopa kufa kutokana na maisha anayoacha ( familia,marafiki)

Sasa wadau naomba michango yenu kwa mtazamo wako au nafsi yako unaona kwanini mtu anaogopa kufa...???

N:B Majibu ya mjadala huu ya siingiliane na imani za dini ila mitazamo huru ya kibinadamu!!
 
Fear of the unknown ndo sababu if you ask me!! Like naweza kulinganisha hii case na maybe this. Imagine kuna vikapu viwili, Kimoja kikiwa na nyoka mwenye sumu kali ya kukuua in seconds huku kingine kiko tupu. Ukipewa option kua ni lazima uweke mkono wako kwenye kikapu kimojawapo, utasita na kuanza kuogopa not because of the poisonous snake(this comes later) maana unajua one of the choice is safe so biggest fear inkua ni kutokujua which busket has the snake. Binadamu ni kiumbe anaetaka kujua whats going on around him mda wote, na ukitaka umtese more ni umfiche na kumwacha hajui wats going on. Ukirudi kwenye kikapu hapo fear anayokua nayo mtu mwenye option mbili inakua ni tofauti na yule atakaeekewa kikapu kimoja tu chenye nyoka, ye anajua wats the outcome and goes in prepd tofaut na wa kwanza. So the biggest fear is not knowing what comes and that if you make a wrong choice you're doomed! Thats wat i think
 
Je kwa watu ambao wanajiua inakuaje?, pia hiyo fear of the unknown naona hadi uwe unaamini kuna after life?
 
Na wanaojiua wanaogopa kufa?

Kwa mtazamo wangu hawaogopi kutokana tayari wamekata tamaa ya hali ya maisha yao, au wanataka tu escape ya hatma zao kimaisha.Kufa ndio last resort ya maisha yao
 
Siogopi kfa lakini naogopa matokeo na athari za kifo changu kwa jamii. Familia itaishije na maisha yao yatakuwaje, nani ataziba na kwa vipi ataziba pengo naloacha? Na kuhusu wale niliowapenda na plans nilizotumia miaka kuzijenga na kuzifanya kuwa halisi? Hapo ndio kitendawili
 
Kwa hiyo fear yako sio ya after life, je ukipewa option lini utakua tayari kufa in terms ya miaka utaweza sema.
 
Je kipi kinachofanya tunaogopa kufa ingawa tunajua lazima tufe
 
Kwa hiyo fear yako sio ya after life, je ukipewa option lini utakua tayari kufa in terms ya miaka utaweza sema.

at least 80 and about after the facts are still unclearly disclosed. I think everlasting fire ni theory
 
Na wanaojiua wanaogopa kufa?

Mkuu The Boss, japo mleta uzi ameweka limitations kuwa maoni ya wana jamvi yasiingiliane na imani za kidini; hakika ninaamini kuwa dini ina play a great role ktk baadhi ya wale wanaojiua (au kuua). Pia kitu kingine ni kukata tamaa kama wengine walivyosema hapa jamvini; binadamu akishakata tamaa, kwa kawaida hawezi kufikiri lolote lile lililo hapa duniani au litakalo tokea mbele ya safari.
 
Last edited by a moderator:
Jamani wadau katika pita pita zangu nilijikuta katika mjadala mkali kuhusu kifo, Mjadala ulikua hivi:

1. Je watu wanahofia kufa kwa sababu ya uoga wa kutojua mbele kuna nini? (motoni na peponi) au
2. Watu wanaogopa kufa kutokana na maisha anayoacha ( familia,marafiki)

Sasa wadau naomba michango yenu kwa mtazamo wako au nafsi yako unaona kwanini mtu anaogopa kufa...???

N:B Majibu ya mjadala huu ya siingiliane na imani za dini ila mitazamo huru ya kibinadamu!!

Watu hawaogopi KUFA bali wanaogopa KUTANGULIA

Seriously, kama umepoteza sababu ya kuishi (mzee sana, mke au mume na rafiki zako wote wamekwisha kufa, una maradhi yasiyotibika, familia yako haioni umuhimu wako tena, nk) basi kifo hakitishi tena BALI namna utakavyokufa (kuliwa na simba, kugongwa na gari, au kufa peacefully usingizini) ndicho kitu kinachowatia watu wengi mtera.

Bila ya kuingiza udini, IMANI yako inaweza kukusaidia sana katika kujitaarisha kufa.
 
Tunaogopa vyote.Mchakato wa kufa kwa maana tunawaza maumivu ya ugonjwa,ajali,na huyo tunaeambiwa mtoa roho kuwa anatisha.Pili tunaogopa yatakayokuja baada ya kufa.Kwa waliouguza ndugu zao au watu wao wa karibu ni mashahidi tosha siku wapendwa wao wanakata roho walishuhudia vibweka,mara mwingine haja kubwa na ndogo zinamtoka,mwingne macho anatoa sana na kurusha mikono na miguu kwa nguvu.Hzo ni dalili kuwa process nzima ya kufa syo ya kitoto.Ni suala zito
 
Kwanza mi nahitaji kujua kufa au kifo kwa mantiki ya kufa ni nini? Pia kitu gani au kiashiria cha kifo ni kipi?
 
mimi kwa kweli naogopa,just because wanangu watalelewa na nani?lakini nikifikisha miaka 100 hivi,wala siogopi
 
Watu hawaogopi KUFA bali wanaogopa KUTANGULIA

Seriously, kama umepoteza sababu ya kuishi (mzee sana, mke au mume na rafiki zako wote wamekwisha kufa, una maradhi yasiyotibika, familia yako haioni umuhimu wako tena, nk) basi kifo hakitishi tena BALI namna utakavyokufa (kuliwa na simba, kugongwa na gari, au kufa peacefully usingizini) ndicho kitu kinachowatia watu wengi mtera.

Bila ya kuingiza udini, IMANI yako inaweza kukusaidia sana katika kujitaarisha kufa.
Kwahiyo kikubwa ni watu au maisha yako unayoacha ndio yanakutia hofu ila sio suala la motoni au peponi?
 
Back
Top Bottom