Kwanini unapaswa kufuta Vidakuzi 'Cookies' vya Kivinjari Chako Mara kwa Mara

Kwanini unapaswa kufuta Vidakuzi 'Cookies' vya Kivinjari Chako Mara kwa Mara

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Vidakuzi ni data zinazokusanywa na tovuti unazotembelea na kuhifadhiwa kwenye kivinjari chako, zikijumuisha taarifa kuhusu shughuli zako kama kurasa ulizotembelea na muda uliokaa kwenye tovuti.

1726520311972.png
Jinsi ya kufuta Vidakuzi 'Cookies' vya Kivinjari Chako

a. Safari (Mac): Nenda Preferences > Privacy > Manage Website Data > Remove All.

c. Firefox: Nenda Options/Preferences > Privacy & Security > Cookies and Site Data > Clear Data.

d. Google Chrome: Nenda kwenye Settings > Privacy and security > Clear Browsing Data > weka alama kwenye Cookies and other site data > Clear data

Kwanini Ufute Vidakuzi 'Cookies' vya Kivinjari Chako:
  • Kuongeza kasi ya mtandao
    Baada ya muda, cookies zinapokusanyika kwa wingi, zinaweza kusababisha mifumo yako kupungua kasi. Hii ndiyo sababu wataalamu wa IT wanapendekeza kufuta cookies unapokumbana na matatizo ya kasi ya mtandao.

  • Unapotumia kompyuta ya pamoja
    Ni muhimu kufuta cookies unapomaliza kutumia kompyuta ya pamoja au ya umma ili watumiaji wengine wasiweze kufikia taarifa zako, au kutumia tovuti wakiwa wameingia kwenye akaunti zako. Kutokana na uwepo wa cookies, mtumiaji mwingine anaweza kuona historia yako ya kutumia kompyuta au kununua/kufikia taarifa akiwa kwenye akaunti yako kwenye tovuti mbalimbali (kama vile za biashara, benki, mitandao ya kijamii, na barua pepe).

  • Kujilinda dhidi ya uhalifu mtandaoni
    Kwa bahati mbaya, wahalifu wa mtandao wanaweza kupata data iliyohifadhiwa kwenye cookies na kuiba taarifa zako binafsi. Taarifa hizi zinaweza kuuzwa kwa faida au kutumika kufanya manunuzi mtandaoni au kufikia akaunti za benki.

  • Kuepuka matangazo yanayolengwa
    Moja ya sababu kuu kwa nini watumiaji wa intaneti huchagua kufuta cookies ni kuzuia matangazo yanayowalenga yasiwafuate kila wanapotumia mtandao. Cookies za wahusika wa tatu zinazorekodi vitu ulivyoviona mtandaoni zinaweza kuwa kero kubwa kwa watu wengine, ambao hawapendi kuona matangazo yanayojirudia kila mara wanapotumia intaneti.
Soma Pia: Unatumia Mbinu gani kuimarisha Usalama wako Mtandaoni?
 
Back
Top Bottom