Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kwanini mwanaume anapokuwa na malengo ya kudumu na Mwanamke - ghafla mwanamke huanza kuonyesha tabia za ajabu ajabu,mara haeleweki anataka nini,mara simu hapokei, sms hajibu,anakuwa mkali sana kwa vitu vidogo vidogo,anakuwa na majibu mabaya mara kwa mara?
vilevile kwa nini mwanamke mwenye malengo ya kudumu na mwanaume huwa anaparamia mwanaume ambaye hana malengo naye?
ZIFUATAZO NI SABABU 3 ZENYE KUFANYA MWENZA WAKO ANAKUTESA SANA UKIWA NA MALENGO NAYE
Sababu hizo 3 ni kama ifuatavyo
1.UNATAKA KUMLEA KAMA VILE MZAZI WAKE
Mzazi huwa anapenda kumpa onyo mtoto, kumgombeza, kumkaripia,kumpiga,kumpa tahadhari mara kwa mara kwa lengo la kuhakikisha usalama wa mtoto.
Vilevile kwa wanaume au wanawake wengi wakiwa na malengo ya kudumu na mwenza huwa wanageuka kuwa wazazi badala ya kuwa mwenza.
Utajuaje kama umegeuka mzazi kwa mwenza wako
a.Tabia ya ukosoaji kupitiliza mara kwa mara unakuwa unamkosoa mwenza wako kwanzia uvaaji, utembeaji, ulaji, matumizi ya fedha,kumpangia marafiki, kumuelekeza nini cha kufanya saa 24, kumrekebisha tabia mara kwa mara,kumuona mwenza wako hana akili timamu za kujiongoza wala kufanya maamuzi.
Hakuna mwanaume au mwanamke ambaye anapenda kuishi na Mwenza mkosoaji kupitiliza inakuwa kero,mtu kuongea kitu kidogo masaa 2 mfululizo,mtu kutoa vitisho na tahadhari muda wote,mtu kukupa ushauri saa 24 inakuwa kero.
b.Kubeba majukumu ya Mwenza wako
hapa mara nyingi wanawake wengi huwa wanakosea.Mwanamke anafanya kazi zote za nyumbani kama kupika, kufua,kufanya usafi,kutunza watoto kisha anabeba majukumu yote ya mwanaume kama vile kujenga, kufungua biashara, kumtafutia kazi, kumchukulia mkopo mwanaume wake,kumpa mtaji mwanaume lakini mwanaume anakula mtaji,
wakati huohuo mwanaume kazi yake ni kulewa, kubadilisha wanawake kama nguo,mwanaume kazi yake kumuingilia kinguvu,kumpiga, kumdhalilisha, kumtukana.
Amani haipatikani kwa kubeba majukumu yote ndani ya familia bali kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa kubeba majukumu yake ipasavyo bila kuingilia mipaka ya mtu mwingine.
2.UNATAKA AKUPENDE SANA KULIKO KITU CHOCHOTE
Sababu ya pili yenye kufanya mwenza wako anakutesa ni kwamba unataka akupende.
Mapenzi hayana bima wala guarantee yanaweza kuwepo leo kesho unakuwepo uadui.
Mapenzi ni hisia na hisia huwa zinakuja na kuondoka.
Kosa kubwa sana ambalo Watu wengi huwa wanafanya ni kutaka maisha ya honeymoon kila siku miaka yote haiwezekani.Maisha hayo yapo kwenye movies na tamthilia tu.
Mtu yeyote akiona unataka akupende ili uwe na furaha lazima atakupanda kichwani,kwanza hawezi kukuheshimu, vilevile atakupuuza,atakuona takataka, atakuona bwege, atakuona lofa,atakuona haujielewi kwa sababu anakuwa hafanyi kazi yoyote ya kukufurahisha lakini wewe unakuwa unajitutumua kumfurahisha saa 24 ili akupende.
Kwa Mwanamke kutaka kupendwa ni sahihi lakini kwa mwanaume ambaye anataka kupendwa anakuwa na tatizo.Unapotaka kupendwa unapoteza uwezo wa kujiamini mbele ya mtu huyo , vilevile unapoteza uwezo wa kuona makosa na mapungufu ya mwenza wako.
unapotaka kuheshimiwa na mwenza wako inakuwa rahisi kuona makosa na mapungufu yake kisha unakuwa na uwezo wa kukemea tabia mbaya za Mwenza wako.
Mwanaume ni kichwa cha familia hivyo hauwezi kusimama kama kichwa wakati huohuo unataka kupendwa lazima uonekane bwege.
Hata ofisini bosi akiwa anataka kupendwa na kila mtu huonekana DHAIFU vilevile hata uwezo wake wa kufanya maamuzi magumu unatoweka.
Mtu ambaye anataka kupendwa huwa anaonyesha utii na unyenyekevu kwa sababu anakuwa anataka kuongozwa lakini mtu ambaye anataka kuheshimiwa haitaji kuongea kwa kunyenyekea sana bali kuongea kwa sauti nzito yenye mamlaka ndani yake.
3.UNAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA SANA ILI AKUONE WIFE MATERIAL/HUSBAND MATERIAL
Sababu ya mwisho yenye kufanya mwenza wako anakutesa sana kwa sababu upo na malengo naye ni kwamba umefanya uwekezaji mkubwa sana kwake ili akupende.
Mwanaume ambaye huteswa sana kwenye mapenzi huwa anatumia fedha nyingi sana kwa ajili ya kumfurahisha Mwanamke, vilevile anatumia pesa nyingi sana kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama, kumjengea, kusaidia ndugu wa Mwanamke,kusaidia marafiki wa Mwanamke, kuwasomesha watoto wa Mwanamke ambao amezaa na wanaume wengine, kuwasomesha wadogo zake mwanamke, kuwafungulia biashara ndugu zake mwanamke.
Ukweli mchungu ni kwamba Mwanamke yeyote akiona anakula bure, anavaa bure, anatumia simu ya gharama,ananunuliwa zawadi za gharama kubwa sana wakati huohuo hafanyi kazi yoyote ya kumfurahisha mwanaume lazima atamchoka mwanaume kisha atakwenda kutafuta mwanaume wa ndoto zake.
Mwanamke kwa asili huwa mlezi,ndio maana huwa anataka kumbadilisha mwanaume tabia.
Ikitokea mwanaume ni mwema sana,sio mlevi,hachepuki,havuti bangi,anafanya kazi na kurudi nyumbani mapema,mwanaume ni mpole kupitiliza, mvumilivu sana,mwanaume anasamehe makosa haraka ni wazi kwamba Mwanamke ataona ni fursa ya kutoroka kwenda nyumbani kwao kisha atalala na wanaume tofauti tofauti kisha akiwa na ujauzito wa mwanaume mwengine ataona ni fursa ya kurudi kuomba msamaha,anajua atapata nafasi nyingine tu.
Mwanamke huwa anafanya uwekezaji mkubwa sana pale ambapo anakuwa na hofu ya kuachwa mpweke lakini hafanyi uwekezaji wowote kama anajua hauwezi kumuacha wala hauwezi kuishi bila yeye.
Upendo wa Mwanamke upo kwenye jasho lake sio kwenye uwekezaji ambao mwanaume anafanya .
Mwanaume anapofanya uwekezaji mkubwa sana kwa Mwanamke ni wazi kwamba ambaye anakwenda kulia siku za karibuni ni mwanaume.
Mwanamke akifanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwanaume anakuwa hana mpango wa kuachana na mwanaume husika.
Hii ndio sababu badala ya kufanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwenza wako fanya uwekezaji mkubwa sana kwako wewe mwenyewe.
Tumia 90% ya fedha zako kufungua biashara zako,kuvaa vizuri,kula vizuri, kutembelea sehemu zenye kuvutia,nunua usafiri wako,nunua simu ya gharama tumia wewe sio mwenza wako,
Hakikisha kabla mwenza wako hajapendeza kwa fedha zako wewe vaa vizuri sana ili akiondoka akuache ukiwa na muonekano mzuri sana wa kuvutia Watu wengine.
Hakikisha mwenza wako anapendeza kwa jasho lake kwa maana ukiwa mwanaume unamhudumia pale ambapo anaonyesha utii na, unyenyekevu na heshima tu kama haonyeshi vitu hivyo huduma kwake hakuna.
Mapenzi yanauma sana kama umeachwa umekonda, umepauka,unanuka, hauna kazi wala biashara,hauna afya isipokuwa umebaki mgonjwa tu.
Kabla ya kuboresha maisha ya mwenza wako hakikisha maisha yako ni mazuri sana.
Mwenza wako atumie 10% tu ya fedha zako ili hata ukimfumania au akiondoka akuache ukiwa na maisha mazuri sana.
Epuka kufanya uwekezaji mkubwa sana kwa mwenza wako kama uthibitisho wa mapenzi ya dhati utajuta.