Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Kisaikolojia kuna falsafa inaitwa "Monkey branch" ambayo inaeleza kwamba ni hali ya mwanamke/mwanaume kuamua kuanzisha mahusiano mapya wakati huohuo anakuwa kwenye mahusiano ya kudumu ambayo hayana migogoro hata kidogo.
Kwa maana kwamba mwanaume au mwanamke anakuwa anatafuta changamoto mpya nje ya mahusiano yake yenye amani, furaha na utulivu.Kwa maana mwenza mmoja anakuwa na mahusiano mapya wakati mahusiano ya awali hayana dosari yoyote.
Kwanini watu huanzisha mahusiano mapya wakati wapo kwenye ndoa/mahusiano yenye amani , furaha na utulivu?
Jibu lake ni kwamba mwanaume au mwanamke yeyote pale ambapo anapokuwa na uhakika kwamba unampenda sana kuliko mtu yeyote hapa ulimwenguni na vilevile upo tayari kufa kwa ajili yake unakuwa unampa mwanamke/mwanaume wako tiketi ya kwenda kutafuta mwenza wa ndoto zake ambaye atatumia muda mwingi kufurahia naye maisha huku anajua hauwezi kuishi bila yeye,wala hauwezi kumuacha hivyo wewe unakuwa "back up plan".
Mwenza wako anakutumia wewe kwa DHARURA tu ,endapo mahusiano yake na mwenza wa ndoto zake watagombana anakuja kwako kupata faraja na msaada wa kifedha kisha wakiombana msamaha na kuelewana anarudi kwa mwenza wa ndoto zake huku anasubiri ugomvi mwengine aje kwako kupata faraja na msaada wa kifedha.Hali hiyo ya wewe na mwenza wako kuachana na kurudiana inakuwa yenye kujirudia rudia kutegemea na mahusiano baina ya mwenza wako na yule mwanaume au mwanamke wa ndoto zake.Wakiwa na amani wewe unakuwa mpweke kupitiliza,wakiwa na ugomvi inakuwa zamu yako kumpa faraja, kumliwaza, kumbembeleza,kumsaidia fedha.
Tabia ya mwenza wako inakuwa ANAKUACHA kimyakimya ghafla bila kukupa taarifa (Ghosting),kisha baadaye anakuja kwako,kisha anaondoka zake ghafla,baada ya mwezi,au miezi kadhaa kupita anarudi kwako kuhakikisha kwamba hauna mwanamke au mwanaume mpya.
Kwa sababu utakuwa na hisia kali sana za mapenzi juu yake unakuwa hauna ujanja wa kumuacha kwa sababu akija kwako unakuwa na matumaini ya kudumu naye kisha anakuacha ghafla.
VIASHIRIA VYENYE KUONYESHA KWAMBA MWENZA WAKO ANATAKA KUKUTUMIA KAMA TAMBARA LA DEKI-ANAKUACHA GHAFLA BILA SABABU KISHA ANARUDI KUOMBA MSAMAHA KISHA ANAKUACHA TENA
Pale ambapo mwenza wako anataka kukutumia kama tambara la deki kwa maana anataka uwepo wako utumike kwa maslahi yake binafsi kisha akuache mpweke kisha arejee kwako kuomba msamaha ,kutishia kujiua, kusingizia shetani alimpitia, kukubembeleza, kusingizia alirogwa, kusingizia alikuwa na "stress" -
Mwenza wako ataonyesha tabia zifuatazo
1.KUJITENGA GHAFLA BILA SABABU ZOZOTE ZA MSINGI
Mwenza kama anataka muachane kisha aje baadaye kukutumia kama tambara la deki,kisha ukimpa faraja na msaada wa kifedha aondoke tena kwenda kwa mwanamke au mwanaume wa HADHI yake,basi atakata mawasiliano ghafla wakati haujafanya kosa lolote,utapiga simu hapokei,ukituma sms hajibu,utaomba msamaha wakati haujafanya kosa lolote lakini haonyeshi ushirikiano wowote,ukimfuata kazini kwake au sehemu anapoishi bila taarifa hakupi ushirikiano wowote.Atajifanya mwenye hasira kupitiliza,atajiweka mbali na wewe,atanuna, anasusa, atagoma kulala na wewe,atakuwa na visingizio kibao kukukwepa.
2.ATAKUWA NA SIRI SANA KULIKO KAWAIDA YAKE
Mwenza anapotaka mahusiano kuvunjika kisha anarudi kwako kuomba msamaha kusingizia shetani alimpitia ataanza kufanya mambo ya ajabu ajabu.
Ataweka password mpya ukiuliza tu atakugeuzia kibao,ataibua ugomvi bila sababu zozote za msingi, anakuporomoshea matusi ya nguoni,atachelewa kurudi nyumbani tofauti na mazoea yake, anaweza kuanza kununua vitu kwa siri kama vile kujenga kwa siri, kufungua biashara kwa siri,atakuwa na matumizi ya fedha tofauti na hapo awali,mipango yakehaiweki wazi.Utamshirikisha kwenye mambo yako lakini yeye atakuwa msiri sana kuliko kawaida.
3.ATAKUWA ANAKUKOSOA KUPITILIZA BILA SABABU ZOZOTE ZA MSINGI
Mwenza wako anapotaka muachane ataanza kukosoa vikali sana muonekano wako, lafudhi yako,tabia zako, vipaumbele vyako,uwezo wako wa kiakili,atakashfu kabila lako na familia yako lengo ujichukie muachane.
4.VIPAUMBELE VITABADILIKA
Mwenza wako anaweza kuonekana mwenye hobbies mpya tofauti na hapo awali,mwenza wako atakuwa na marafiki wapya tofauti na hapo awali, mabadiliko ya tabia za mwenza wako yatahusisha mwenza wako kukwazika na kila kitu kuhusu wewe,akikuona anakuwa na hasira kupitiliza kuliko kawaida yake.Ukiondoka anakuwa na furaha sana.Anataka ukaribu na wewe pale ambapo anashida tu kama hana shida hataki umsogelee.
5.MWENZA WAKO ATAKWAMISHA MAHUSIANO YENU KWA MAKUSUDI
Kama mwenza wako anataka muachane lakini anataka baadaye aje kwako kupata faraja na msaada wa kifedha ataanza kupunguza ukaribu na wewe,atakata mawasiliano ghafla,kisha atakuwa anaibua ugomvi bila sababu zozote za msingi.
Kama ukiuliza kuhusu hatima ya mahusiano yenu hakupi majibu ya kueleweka, ukiuliza lini mtaonana kama mnaishi sehemu tofauti atasema nitakwambia lakini hasemi hata kwa miezi minne bado jibu lake linakuwa vilevile kuwa atakwambia siku ya kuonana lakini hasemi.
-Atakuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wako lengo ushindwe kumpa fedha aondoke kwenda kwa mwenza wa ndoto zake lakini baadaye atarudi kusingizia shetani alimpitia.
Kama unataka ndoa basi atakuwa na visingizio kibao kukwepa mada ya ndoa,kama unataka akutambulishe nyumbani kwao atakuwa na visingizio kibao kukwepa mada hiyo,ukitaka kumtambulisha kwa wazazi wako anakuwa na hasira kupitiliza pamoja na dharura za mara kwa mara lakini pesa zako anataka ukisema hauna fedha ananuna, anaanza kulalamika kwamba haumpendi.
Utaongea kwa makini sana kuepuka kumkasirisha lakini anakuwa na hasira kupitiliza akiona sura yako.