Asha Hincha
Member
- Jul 13, 2021
- 15
- 18
Rejea picha hapo juu
(picha kutoka mtandaoni)
Hayo ni makubaliano ambayo unahitajika kusaini kabla ya kupokea chanjo, kwamba uko tayari kwa lolote lile litakalo tokea na serekali haito wajibika.
Je, hii ina maana gani?
Je, ni kwamba Serekali haina imani na chanjo hiyo?
Au wanafahamu wao kwamba chanjo ina madhara?
Ufafanuzi wa hili,
Tuchukue mfano wa matibabu yanayo hitajika kufanyiwa upasuaji, kabla ya kuingia kwenye upasuaji utasaini makubaliano kwamba upo tayari na lolote litakalo tokea hata kama ni kifo, kwanini?
kwasababu upasuaji hauna guarantee, matokeo yake hayatabiriki kwamba utafanikiwa au utapoteza maisha.
Kwa maana daktari atawajibika kufanya kadiri ya uwezo wake lakini hatuwezi kuyatabiri matokeo yake, kitu pekee ni daktari atawajibishwa endapo tu atafanya uzembe wa wazi,
Hivyo mgonjwa utachagua kwa hiyari yako.
Kwa upande wa chanjo,
kwa kawaida chanjo ili ithibitishwe kwa matumizi ya binadamu lazima ifanyiwe majaribio katika hatua nne ama tano
1.Discovery and development (laboratories)
2. Pre clinical trials(laboratories)
3.clinical trials(health settings)
4. Regulatory authorities evaluations
5. Post market monitoring
Hatua hizi zinachuka jumla ya miaka kumi au zaidi mpaka kukamilika, mpaka dawa au chanjo kuidhinishwa kwaajili ya matumizi na kuwa na uhakika kwamba chanjo hiyo ni salama na kama kuna matatizo yoyote yanayo ambatana na chanjo hiyo yanakuwa yana fahamika na namna ya kuyashughulikia.
Tunafahamu kwa chanjo nyingine zilizopo huna haja ya kusaini makubaliano, kwasababu zimefanyiwa tafiti tayari na majaribio ya kutosha na zimepitia hatua zote, na lolote litakalo kutokea serekali itawajibika.
Lakini chanjo ya COVID-19 imechukua takribani mwaka au miaka miwili tu mpaka kuingia sokoni na kuanza kutumika.
Tufahamu kwenye taratibu za kiafya kuna kitu kinaitwa dharura, isinge wezekana kusubiri chanjo zifanyiwe majaribio mpaka miaka 10-15 ndiyo watu waanze kutumia, hivyo inabidi tu ipitie hatua muhimu za mwanzo na kuingia sokoni kutumika huku tafiti zikiendelea, kwa maana licha ya COVID-19 vaccine kuingia sokoni lakini bado ipo katika majaribio hivyo salama yake na hatari yake baada haija fahamika,pia mamlaka na taalamu ya afya kiujumla hawana jibu la moja kwa moja kama ni salama au si salama na itachukua muda kupata majibu hayo kama nilivyoeleza hapo awali.
Hivyo basi chanjo ya aina hii huwa ni hiyari ya mtu, na pia inashauriwa zaidi kwa watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi (wazee, wenye matatizo mengine ya muda mrefu) lakini pia ukubaliane na matokeo yoyote yale baada ya kupata chanjo na Serikali haito wajibika kwa lolote.
SHUKRANI.
Upvote
11